Mafuta ya Mzeituni/olive oil

Mafuta ya mzeituni au olive yanapatikana baada ya kukamuliwa kwa matunda ya mzeituni. Mizeituni inapatikana zaidi katika nchi za Italia, Hispania na Ugiriki. Ubora wa mafuta haya mzeituni unategemea na aina ya udongo, mazingira ya uzalishaji pamoja na uvunaji wake, kwahivo ladha pamoja na rangi ya mafuta inaweza kutofautiana kulingana na wapi mafuta hayo yamezalishwa, na kiujumla mazingira yenye joto hutoa mafuta mazuri zaidi.

mafuta ya mzeituni
mafuta ya zeituni

Kuna Makundi Manne ya Ubora wa Mafuta ya Mzeituni

  • Extra virgin olive oil; hii ndio gredi ya kwanza ya mafuta yana vitamin za kutosha na hayajaongezewa kemikali mbaya. Tumia aina hii ya mafuta ya mzeituni
  • Pure olive oil; haya huzalishwa kwa kuchanganya mafuta gredi ya kwanza na mafuta yaliyosafishwa kwahivo siyo mazuri kutumia
  • Light olive oil; ni mafuta yaliyosafishwa zaidi na kuwa mepesi yasio na ladha, epuka aina hii ya mafuta ya mzeituni.
  • Olive-pomace oil; aina hii ya mafuta huzalishwa kwa mabaki ya zeituni baada ya gredi ya kwanza kuondolewa. Kemikali nyingi hatarishi (solvents) zinatumika ili kupata aina hii ya mafuta, hakikisha unaepuka aina hii ya mafuta ya mzeituni kwa gharama yoyote.

Faida za Mafuta ya Mzeituni

Mafuta ya mzeituni kama yakitumika vizuri yanaweza kuleta matokeo makubwa sana kwenye afya yako na kukusaidia kwa changamoto hizi

  • Kutibu kisukari cha ukubwani (type 2 diabetes); Tafiti zinasema kwamba mafuta ya olive yakitumika kwa muda mrefu husaidia kupunguza athari ya kisukari na kuimarisha afya ya mgonjwa.
  • Kuimarisha afya ya moyo; kwa kurekebisha shinikizo la damu, kupunguza mafuta mabaya kwenye mishipa ya damu (LDL) na pia kupunguza hatari ya damu kuganda kwenye mshipa ya damu.
  • Kupunguza hatari ya kupata saratani: Ukitumia mara kwa mara mafuta ya mzeituni unapunguza hatari ya kuugua saratani ya matiti na pia kiambata cha oleic acid kilichopo kwenye mafuta haya husadia kupambana na saratani.
  • Kupunguza hatari ya kupata ugonjwa unaoshambulia ubongo (Alzheimer’s disease)

Je Mafuta yako ni feki?

Katika uchaguzi wa mafuta ya olive ni muhimu sana kuwa makini kwani mafuta mengi yanayouzwa ni feki na yamejaa kemikali hatari kwa afya yako. kama mafuta yako ni feki utaona harufu hizi;

  • Harufu ya karanga zilizoharibika na ladha kama ya grisi
  • Harufu ya kuchacha au harufu ya uvundo kama sox zilizovaliwa
  • Harufu ya vumbi au fangasi
  • Harufu ya vinegar/siki
Unaweza kututafuta tukusaidie kukuchagulia na kukupatia mafuta orijino ya mzeituni, ujazo wa lita moja kwa Tsh 35,000/= 

Jinsi ya Kutumia mafuta ya Mzeituni/olive

Mafuta ya olive yanaweza kuongenezwa ladha kwa kuweka viungo mbalimbali na kukaa kwa siku 10 kisha ukaanza kutumia, mfano ukaweka pilipili kwenye mafuta. Mafuta ya mzeituni ni vizuri yatumike yakiwa mabichi, yaani yasichemshwe kabisa kwani yakipata moto hutengeneza kemikali ambazo siyo salama kwa afya, badala yake nyunyiza kwenye chakula chako kabla ya kula.