Kunuka Jasho na Kutokwa Jasho jingi

kunuka jasho

Nini kinapelekea jasho jingi na kunuka jasho kama Mbuzi?

Kutokwa jasho jingi na kunuka jsho sio tu ni tatizo kubwa, bali pia linaweza kuleta aibu. Kwani inasababisha harufu mbaya na kushindwa kujiamini kwa mtu anayekabiliana nalo. Jasho jinsi husababishwa na kutofautiana kwa homoni, matatizo ya neva, na dawa fulani.

Mazoezi ya mwili pia husababisha jasho kubwa, ingawa hii ni njia nzuri ya kuondoa sumu kutoka mwilini. Mbali na hayo, ktokwa jasho bila sababu ni tatizo ambalo linahitaji kudhibitiwa ili urudishe furaha yako. Hapa chini kuna tiba za nyumbani zinazoweza kutumika kwa matibabu kabla ya kujaribu njia zingine zenye kemikali.

1.Majani ya chai

Majani ya chai pia yanaweza kusaidia kupunguza jasho kubwa . Kiambata cha Tannins kilichopo kwenye majani ya chai ndicho kitakupa matokeo haya. Majani ya chai yanaweza kutumika kama maji baridi ya kuweka mwili wako baridi na kuzuia jasho kubwa. Weka vijio viwili vikubwa vya majani ya chai kwenye chombo cha maji ya uvuguvugu. Ruhusu maji yachanganyike na yawe joto la kawaida. Loweka mwili wako kwenye maji haya kwa nusu saa kila siku ili kudhibiti jasho.

2.Nyanya

Nyanya zina antioxidants(yaani viondoa sumu) na hii ina metokeo mazuri kwenye mwili mzima ikiwa ni pamoja na tezi za jasho, ambazo pia zitadhibitiwa na matibabu. Chukua nyanya 2-3 kila siku, ondoa mbegu zake na utengeneze juisi yake. Kunywa glasi tatu za juisi ya nyanya baridi ni matibabu yanayopendekezwa kwa jasho kubwa. Baada ya wiki tano ya matibabu na juisi ya nyanya, utaona tofauti kubwa kwenye dalili zako. Sasa, unaweza kupunguza matumizi ya juisi hadi mara moja kwa siku baada ya kupata matokeo chanya.

3.Apple cider Vinegar

Kutumia vinegar ya apple kwenye maeneo yanayotoka jasho kwa wingi inajulikana kama dawa ya kuondoa jasho. Vinegar ama siki hufunika ngozi na vishimo ambavyo jasho hutoka kwa wimgi. Matumizi: Chukua kiwango kidogo kwa kutumia pamba, weka kwenye maeneo yanayotoka jasho sana kama kwenye kwapa. Jipe muda ili vinegar iweze kukauka, na ufanye zoezi hili mara mbili kwa siku asbhi na jioni baada ya kuoga.

4.Green tea

Green tea inaongeza kiwango cha shughuli za mwili na husaidia kutolewa kwa mafuta na sumu kwa urahisi kupitia kinyesi. Pia ni dawa ya kupunguza msongo. Kunywa vikombe 2-3 vya green tea kila siku inaweza kusaidia kudhibiti jasho kwa kiasi kikubwa. Kwa sababu ya kutolewa kwa taka sumu kwa kiwango kinachofaa kwenye mwili, jasho kubwa litadhibitiwa kwa kiasi kikubwa na hautahitaji kuhangaika tena wala kuaibika.

5.Baking soda

Baking Soda ya kuoka mandazi ina uwezo mkubwa wa kufyonza majimaji na inaweza kutumika kwa kusugua kwenye maeneo yanayotoka jasho. Hii itadhibiti jasho na kukusaidia kuwa mkavu. Matumizi: Asubuhi ukishaoga kabla hujaenda kwenye mizunguko yako jipa