Mafuta ya Mkaratusi yanatokana na nini?
Mafuta ya mkaratusi haya hupatikana baada ya kukaushwa kwa majani mkaratusi, badae majani haya yakapitishwa kwenye joto na mafuta yanayopatikana kukingwa na kupozwa kwa kutumia vifaa maalumu. Tafiti zinasema kwamba kuna aina zaidi ya 700 za miti ya mikaratusi na kati ya hiyo aina 500 ndizo zinaweza kutoa mafuta tiba haya.
Kwa miaka ya zamani mafuta yalitumia kutibu maumivu na kupunguza kuvimba kwa mwili, kwa miaka ya sasa mafuta haya yamegundulika kuwa na uwezo mkubwa zaidi na kutibu changamoto nyingi zaidi na hata kutumika kutengeneza pafyum na marashi mengine.
Matumizi ya Mafuta ya Mkaratusi
- Mafuta ya eucalyptus yanasaidia kutibu changamoto za kikohozi kikali, na maambukizi kwenye njia ya hewa.
- Kutibu majeraha na vidonda: hii ni kutokana na uwezo wake wa kuua vimelea hasa bakteria, tumia kwa vidonda, jeraha la kuungua moto, jeraha la kujikata na kitu cha ncha kali, ama jeraha la kunag’atwa na mdudu.
- Mafuta yanatumika pia kuua vimelea wabaya kama bakteria, virusi na fangasi.
- Kupunguza maumivu makali ya misuli na joints
- Kutuliza akili na msongo wa mawazo
- Kuimarisha ufanyaji kazi wa ubongo na mzunguko wa damu
- Kupunguza maumivu ya masikio: Mafuta haya yanasaidia kufungua njia za kwenye masikio zilizoziba , kuua vimelea kwenye masikio, kutibu maambukizi ya bakteria kwenye masikio na hivo kuondoa maumivu makali kwenye masikio.
Namna ya kutumia Mafuta ya Mkaratusi
Namna ya Kutumia mafuta ya Eucalyptus
Mafuta haya unaweza kutumia kwa namna nyingi kwa kulingana na mazingia yako kama
- Kwa ajili ya kuimarisha usingizi chovya kiasi kidogo cha mafuta kwa kutumia pamba na kuweka puani, ama pakaa kiasi kidogo cha mafuta kwenye mto kabla ya kwenda kulala.
- Weka mafuta kidogo kwenye maji ya uvuguvugu kisha oga,
- Kutibu maumivu ya misuli na joints changanya na mafuta mengine mfano mafuta ya nazi, almond au jojoba kisha pakaa taratibu kwenye ngozi .
- Kama unahitaji kufanya masaji changanya kiasi kidogo cha mafuta ya eucalyptus kwenye mafuta unayotumia kufanya massage.
- Kama una maambukizi kwenye njia ya hewa mfano tonslitis au maumivu ya fizi na jino chukua maji ya uvuguvugu weka mafuta kidogo kisha sukutua kwenye eneo la koo bila kumeza.
Je mafuta ya Mkaratusi ni salama?
Mafuta tiba ya eucalyptus ni salama kutumia lakini hakikisha unachukua tahadhari pia. Kama ngozi yako ina aleji na mafuta haya, ama unapata muwasho ama kuvimba wa ngozi pale unapotumia, yatakiwa usitishe kutumia.
Mafuta ya eucalyptus hayatakiwi kutumiwa na watoto hasa wa umri chini ya miaka miwili. Wanawake wajawazito na wanaonyonyesha pia hawashauriwi kutumia mafuta haya.
Muhimu:Usimeze mafuta ya eucalyptus, na pia unapotumia mafuta kwa kupaka kwenye eneo la ngozi hakikisha unachangaya na mafuta mengine kama mafuta ya nazi, olive, almond au jojoba, kwnaini ufanye hivo? kwasababu mchanganyiko huu unasaidia kuongeza ufyonzaji na pia mafuta kuwepo kwa muda mrefu kwasababu mafuta ya eucalyptus yanayeyuka mapema.