Aloe vera ni mmea unaoweza kudumu kwa zaidi ya misimu miwili baada ya kupandwa, unapatikana hasa katika maeneo ya joto na yenye mvua kidogo.
Kwa miaka mingi mmea wa aloe vera umekuwa nguzo ya kutatua magonjwa mengi duniani. Ikipatikana katika mfumo wa juisi, vidonge na mafuta ya aloe vera.
Misri ya kale inaaminika kwamba walitumia mimea hii kutibu maambukizi mbalimbali, vidonda na majeraha ya moto.
Waarabu na wagiriki wa kale walitumia mmea wa aloe vera kuondoa harufu mbaya mwilini. Unaweza kujionea ni kwa kiasi gani mmea huu ulivo na maajabu mengi katika kutibu magonjwa na changamoto mbalimbali.
Faida na matumizi ya Mafuta ya Aloe Vera
- Masaji ya mwili ili kupunguzua maumivu ya joints na misuli
- Kutibu uvimbe baada ya kung’atwa na mdudu
- Kuimarisha afya ya kinywa: mafuta ya aloe vera ni tiba kwa magonjwa ya meno kama kuoza meno, harufu mbaya kwenye kinywa na kuvimba kwa fizi.
- Kutibu chunusi na kupambana na hali ya kuvimba kwa uso, mapunye na muwasho wa ngozi. Aloe vera pia inatibu haraka ngozi iliyoharibika kwa kuungua na jua.
- Kuondoa michirizi na makovu yanayotokana na uzito mkubwa ama athari za chunusi.
Jinsi ya Kutengeneza Mafuta ya aloe Vera ukiwa Nyumbani kwako.
Mafuta ya aloe vera yanatengenezwa kwa kuchanganya vipande vya mmea wa aloe vera pamoja na mafuta mengine mfano mafuta ya nazi, mafuta yanapochemshwa yanafonza viambata vya aloe. Baada ya kuchemshwa mafuta huchujwa na kuhifadhiwa kwa matumizi.
Kwa bahati nzuri ni kwamba unaweza kutengeneza mafuta ya aloe vera ukiwa nyumbani kwako. Yafuatayo ni maelekezo namna ya kufanya ili kutengeneza mafuta ya aloe vera ukiwa nyumbani.
MAHITAJI
- Nusu kikombe cha juisi ya aloevera kutoka kwenye mmea
- Nusu kikombe cha mafuta ya nazi
- Kijiko kimoja na mafuta mengine kwa ajili ya kuleta harufu nzuri (hapa tumia mafuta ya rose, peppermint au jasmine)
- Sufuria pamoja na chombo cha kuhifadhia
Hatua za kuandaa Mafuta ya Aloe vera
- Changanya vizuri juis ya aloe vera pamoja na mafuta ya nazi kwenye sufuria lako. unaweza kuongeza nusu kikombe ya juisi na mafuta ya nazi kulingana na uhitaji wako
- Weka kijoko kimoja cha mafuta ya jasmine au peppermint kwenye sufuria lakona uchanganye vizuri.
- Weka mchanganyiko wako kwenye jikola moto wa kawaida kwa dakika kumi isha epua acha mchanganyiko upoe.
- Baada ya kupoa tayari mchanganyiko wako unaweza kutumika kupakaa maeneo mbalimbali ya mwili.
- Hifadhi mafuta yako kwenye friji ili yatumike kwa muda mrefu zaidi.
Je Mafuta ya Aloe Vera ni Salama kutumika na Kila Mtu?
Kabla ya kupakaa mafuta kwenye ngozi yako hakikisha ni salama na hayana kemikali mbaya.
Kabla ya kutumia aloe kwa kumeza ongea na taalamu wa tiba asili akupe ushauri, kwa maana inaweza kusababisha kutapika, kuharisha na kichefuchefu.
Kama ni mgonjwa wa kisukari, mjamzito ama unanyonyesha ongea na daktari wako kwanza kabla ya kuanza kutumia mafuta ya aloe vera