Kukosa choo na choo kigumu kama cha mbuzi ni moja ya matatizo yanayowapata sana watu siku hizi. Hii ni kutokana na kuvurgika kwa mitindo ya maisha. Tatizo hili linajitokeza pale kinyesi kinapokuwa kigumu kwenye utumbo na hivyo kushindwa kutoka kwa urahisi. Kitaalamu tatizo hili huitwa constipation na husababishwa na kutokwa na haja kubwa mara chache na pia sababu nyingine kama vile lishe, mtindo wa maisha, na magonjwa fulani ya mfumo wa chakula.
Kwa kawaida, matatizo mengi ya constipation yanaweza kutibiwa na kupata nafuu kabisa, ingawa kuna baadhi ya hali tatizo laweza kuwa sugu mpaka kusababisha kuzibika kwa utumbo ambao ni hatari kwa maisha.
Aina za constipation(kukosa choo na choo kigumu)
Kuna aina mbili za constipation kwa watu wazima, yaani constipation ya asili (idiopathic) na constipation ya ufanisi wa mwili yaani (functional). Constipation ya asili haiponi vizuri kwa matibabu ya kawaida. Hata hivyo constipation aina ya pili ambayo inatokea kwa watu wengi inapona haraka kwa kufanya mabadiliko madogo kwenye lishe na mtindo wa maisha, na pia kwa mazoezi maalum ya kuimarisha misuli ya nyonga (pelvic).
Nini kinapelekea kukosa choo na choo kigumu.
Tatizo linaweza kutokana na sababu za kuzaliwa nazo na sababu za kimtindo wa maisha. Visababishi vya kawaida vinavyopelekea ukosea choo ni pamoja na
- kujizia kwenda haja mara kwa mara
- unywaji mdogo wa maji na vimiminika na kutotumia vyakula vya asili vyenye kambakamba
- matumizi ya dawa fulani
- kutofanya mazoezi
- matatizo ya homoni ya tezi dume na
- matatizo ya kimwili kwenye eneo la haja kubwa mfano bawasiri
Tiba za Nyumbani za Kukosa choo
Shida ya choo kigmu na kukosa choo inaweza kutibiwa kwa urahisi na ufanisi nyumbani kwa kutumia tiba mbadala. Tiba hizi sio tu zinakupatia nafuu mara moja, bali pia zinalinda afya yako na kuzuia shida kurudi tena.
1.Mafuta ya Zeituni (Olive Oil)
Mafuta haya yanasifika kama mafuta matakatifu yakitumiwa zaidi makanisani na misikitini. Mafuta ya zeituni ni kichocheo asilia cha kufanya upate haja kubwa na kulinda mfumo wa utumbo. Pia mafuta ya mzeituni yanachochea utoaji wa nyongo ambayo ambayo husaidia kumeng’enya chakula vizuri na kutolewa kwa taka. Nyongo inafanya kinyesi kuwa laini na pia inaamsha utando laini wa utumbo, hivyo kuharakisha usafirishaji wa kinyesi.
Unaweza kula kijiko kimoja cha mafuta ya mzeituni asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Kama tatizo ni sugu, umekosa choo hata siku 4 au wiki, chukua kijiko kingine kabla ya chakula cha mchana. Mara tu tatizo likiisha, unaweza kuendelea kula kijiko cha mafuta ya mzeituni asubuhi au kuyatumia katika lishe yako ya kila siku.
2.Asali
Kutumia asali kwa kutibu choo ipo kwenye matumizi kwa karne nyingi. Asali mbichi ni kichocheo cha kiasili cha kuweka unyevunyevu na hufyonza kiwango kikubwa cha maji na hivo kufanya kinyesi kuwa laini sana. Kiwango cha kutosha cha maji kwenye kinyesi kunachochea kupita kwa kinyesi kwa urahisi kupitia ukuta wa utumbo, bila shinikizo au msuguano wowote.
Matumizi: Chukua vijiko viwili vya asali, lamba saa moja kabla ya kifungua kinywa. Unaweza pia kulamba kijiko kimoja cha asali mara tatu kwa siku ili kupunguza tatizo. Asali pia inaweza kunywewa pamoja na kikombe cha maji ya uvuguvugu au kuongezwa kwenye glasi ya juisi ya limau ya uvuguvugu ili kunufaika na faida zake. Hakikisha unatumia asali mbichi na iliyotayarishwa kiasili ili kufaidika na uwezo wake wa kutibu.
3.Mpera (Guava)
Mpera ni mojawapo ya matunda ambayo hayajapata heshima yake kamili linapokuja suala la faida zake za uponyaji. Mpera pia ni kilainisha choo kizuri sana kunatokana na ukweli kwamba mpera una nyuzinyuzi za lishe ambazo huongeza ukubwa na unyevu kwenye kinyesi chako.
Kutokana na uwezo wake wa kushikilia maji, kula mpera pia ni njia ya kuhakikisha utumbo wako na mfumo wa kutoa taka unakusafishwa kikamilifu na hivyo kuzuia kinyesi kuganda. Unaweza kula mapera baada ya milo yako ama ukanywa maji ya majani ya mpera. Ni muhimu kuhakikisha kuwa unachambua mbegu za mpera pia kwani nazo pia zina athari ya laxative. Kumbuka usile mapera kupita kiasi.
4.Juisi ya Ndimu (Lime)
Kunywa juisi ya ndimu kwa kuachanganya na maji ya moto mapema asubuhi, kunasaidia kutibu choo kigumu. Maji ya moto yanaharakisha mchakato wa umeng’enyaji chakula unapokunywa mapema asubuhi. Pia mchanganyiko wa maji ya moto na juisi ya ndimu husaidia kusafisha ukuta wa utumbo kutokana na takataka zote ambazo zingeweza kuwa zimeganda na kusababisha ukose choo ama upate choo kigumu.
Tumia vidonge asili vya Kayam.
Vidonge hivi asili vimekuwa yakitumika kwa muda mrefu huko india kwa ajili ya changamoto mbalimbali kama kukosa choo na choo kigumu, kiungulia na gesi tumboni.
Hivi sasa vidonge hivi yameonekana kutibu magonjwa mengine zaidi kama bawasili, kuharisha na kuimarisha usagaji wa chakula tumboni. Gharama ni Tsh 35,000/= dozi ya week mbili.
Matumizi: Meza kidonge kimoja mchana na kimoja usiku kabla ya kulala ili kutibu tatizo lako la choo kigumu.