Kungumanga au Nutmeg ni kiungo muhimu sana kwenye mapishi, lakini je wafahamu kwamba mafuta ya tunda hili ni tiba ya magonjwa mengi? Tafiti zinaonesha kwamba mafuta ya kungumanga ya kampaundi za phytochemicals ambazo zinaimarisha afya kwa namna mbalimbali
Mafuta ya kungumanga hutengenezwa kwa kupitishwa kwenye joto kwa tunda la kungumanga na kisha mvuke wake na mafuta kutenganishwa. Matunda haya kupatikana zaidi katika nchi za Indonesia, Sri lanka na Malaysia.
Historia inaeleza kwamba wahindi wa kale walitumia zaidi mafuta ya kungumanga kutibu magonjwa ya tumbo, na wamisri wa kale walitumia mafuta haya kutunza miili ya watu waliokufa isiharibike.
Faida na Matumizi ya Mafuta ya Kungumanga/Nutmeg
- Kutibu harufu mbaya kwenye kinywa: mafuta yanapotukika kwa kusukutua yanasaidia kuondoa bakteria wabaya kwenye kinywa ambao ndio chanzo cha harufu mbaya.
- Kuimarisha usingizi: Mafuta ya kungumanga yatakusaidia kuleta usingizi mzuri na kupunguza athari ya msongo wa mawazo
- Kurekebisha homoni na maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi
- Kupunguza maumivu ya vingo na joints, ianwafaa wenye gauti, arthritis na magonjwa mengine ya joints
- Kutibu changamoto za mfumo wa chakula kama tumbo kujaa gesi, kujamba ovyo.
- Kutibu maammbukizi ya bakteria kwenye njia ya mkojo(UTI)
Jinsi ya Kutumia Mafuta ya Kungumanga
- Ili kutibu changamoto za tumbo- chukua kijiko kimoja cha mafuta haya, changanya na mafuta ya nazi au almond kisha fanya masaji kwenye eneo la tumbo kwa daikika 10 mpaka 15.
- Kutibu maumivu- changanya kijiko kimoja cha mafuta ya kungumanga na kijiko na mafuta ya nazi kisha masaji eneo lenye shida
- Kuondoa harufu mbaya mdomoni- weka kijiko kimoja cha mafuta ya kungumanga kwenye maji ya vuguvugu nusu kikombe kisha sukutua na uteme.
- Kuimarisha hali ya ubongo na kupunguza msongo wa mawazo-weka kiasi kidogo cha mafuta kwenye pamba kisha vuta hewa yake
- Kuimarisha usingizi- Weka matone machache kwenye mto wa kulalia kabla hujaenda kulala.
Je Mafuta ya Kungumanga ni salama kwa kila mtu.
Kama ilivo kwa mafuta tiba mengine mafuta ya kungumanga au nutmeg yakitumika kupita kiasi yanaweza kuleta shida. Kumbua kuchanganya na mafuta mengine kama ya nazi, olive au almond kabla ya kuyatumia.
Kwasababu mafuta haya huchochea mwili yasitumike kwa mgonjwa wa kifafa, watoto chini ya miaka 6 na wajawazito pia wasitumie.