Hedhi Kuvurugika

kalenda ya hedhi

Mzunguko wa kawaida kwa mwanamke huchukua siku 28 ukianzia kuhesabau siku ya kwanza kupata hedhi katika mwezi husika mpaka siku ya kwanza kupata hedhi kwa mwezi unaofuata, lakini mizunguko inatofautiana kwa kila mwanamke. Pale ambapo mzunguko wako wa hedhi unachukua zaidi ya siku 35 hapo tunasema kuna tatizo la hedhi kuvurugika.


Hedhi ni matokeo ya kubomoka kwa ukuta wa kizazi ulioandaliwa kushikilia mimba lakini kwa vile mimba haijashika ukuta huu humeguka na kutolewa nje kama damu ya hedhi.
Wanawake huanza hedhi katika kipindi cha kubalehe kuanza miaka 10 mpaka 16 na hedhi huendelea mpaka pale wakifikia menopause(kukoma hedhi) miaka 45 mpaka 55.

Hedhi inapoanza kutoka kwenye balehe inaweza kuchukua mpaka miaka miwili ili mzunguko kukaa sawa. Baada ya balehe hedhi hutengemaa na siku za mzunguko huanza kufanana.
Japo kwa baadhi ya wanawake hata baada ya balehe kupita hedhi haikai sawa na kiwango cha damu inayotoka kinakuwa kidogo ama kingi kupita kiasi hii ndio hupelekea mvurugiko wa hedhi.

Nini kinasababisha Hedhi Kuvurugika?

  • Mchango wa homoni kuvurugika: Homoni au vichocheo vikuu zinazoratibu mpangilio wa hedhi yako ni estrogen na progesterone, inaweza kuchukua miaka mingi kwa homoni hizi kuwa na uwiano sahihi. Vihatarishi amavyo vinapelekea kuvurugika kwa homoni na hatimaye hedhi kuvurugika ni pamoja na
    • Matumizi ya uzazi wa mpango wa kisasa kama sindano, vidonge na njiti
    • Uzito mkubwa kupita kiasi na kitambi
    • Kupungua uzito kupita kiasi
    • Msongo wa mawazo
    • Changamoto za kushindwa kula vizuri na hivo kukosa virutibishi muhimu
    • Mazoezi makali mfano riadha
  • Kuugua maambukizi kwenye kizazi(PID) kwa muda mrefu: endapo maambukizi haya yasipotibiwa mapema yanaweza kuathiri mirija ya uzazi pamoja na kizazi kwa ujumla na hivo kuvuruga mpangilio wa hedhi, soma kwa kina kwa kubofya hapa kuhusu ugonjwa huu wa PID.
  • Vimbe kwenye mayai(polycstic ovarian syndrome);mfuko wa mayai kwa mwanamake huitwa ovary na mifuko hii huwa miwili kushoto na kulia. Kila mwezi mwanamke hutoa yai moja kwenye kikonyo chake katika upande mmoja ili liweze kurutubishwa, inapotokea mayai kugoma kutoka kwenye mfuko ndipo uanageuka kuwa vimbe zenye maji (cyst) zikiwa nyingi huitwa polycyst. Changmoto hii ndio chanzo kikuu cha mwanamke kuvurugikiwa hedhi.
  • Saratani kwenye kizazi inaweza kusababisha mwanamke kupata hedhi nzito sana ama hedhi katikati ya mzunguko wake
  • Matatizo ya tezi ya shingoni (thyroid gland), tezi hii ndio inayoratibu utolewaji wa homoni za estrogen na progesterone, tezi ikipata hitilafu inapelekea kuvurugika kwa homoni na hivo hedhi pia kuvurugika.
  • Kuvimba kwa kiazi(endometriosis): hali hii hutokea pale seli za ndani ya ya mfuko wa mimba zinapota na kutoka nje ya mfuko wa mimba, hali hii hisababisha maumivu makali wakati wa hedhi lakini pia yaweza kusababisha mabaki ya hedhi kwenye kizazi.

Tiba Asili ya Hedhi Kuvurugika kupitia Vidonge Asili vya Evecare.

evecare capsules

Dawa ni asili na imetengenezwa nchini India kupitia mimea ua Ashoka, Asaparagus na lodh tree. Kwa miaka zaidi ya mitano ambayo tumekuwa tukihudumia wagonjwa wetu wa matatizo ya hedhi, tumepokea shuhuda lukuki. Evecare inakuwa na vidonge 30, unameza vidonge viwili kila siku kwa muda wa wiki mbili.

Baada ya kutumia evecare tegemea kupata matokeo haya

  • Homoni kubalansi
  • Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi
  • Hedhi yako kuwa nyepesi ya kawaida
  • Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa na
  • Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba kama wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu.

Bei ya Evecare ni elfu sabini na tano tu 75,000/= Tuandikie whatsapp kwa namba 0678626254 kuanza tiba

Bofya makala inayofuata:Hatua za Kubana Uke uliolegea