Mafuta ya rose hupatikana kutoka na maua ya mmea wa Rose. Miti yake yenye miiba yake inaweza kukua kwa kujitegemea ama ikakua kwa kujizungusha kwenye mti mwingine.
Matumizi ya Mafuta ya Rose
Mafuta ya Rose yanatumika zaidi viwandani katika kuongeza harufu nzuri kwenye uandaaji wa dawa za kupaka, mafuta na biadhaa zingine nyingi.
Mafuta ya Rose yanaweza kutumika kwa kuvuta hewa yake ili kupunguza msongo wa mawazo na uchovu, lakini nakushauri changanya na mafuta mengine kama jojoba na mafuta ya nazi kabla ya kutumia.
Faida kubwa tatu za Kutumia Mafuta ya Rose
- Kuondoa wasiwasi na msongo wa mawazo kwasababu mafuta yanapunguza kasi kubwa ya shinikizo la damu na pia kukufanya upumue taratibu.
- Kupunguza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi na
- Kupunguza dalili mbaya kwa mwanamke aliyekoma hedhi kama uchovu, kukosa hamu ya tendo na kutokwa jasho wakati wa usiku
- Kuimarisha hamu ya tendo; Mafuta ya rose yanaleta matokeo mazuri kwa mwanaume aliyekosa hamu ya tendo kutokana na msongo wa mawazo na sonona, mafuta yanasaidia pia kurekebisha mpangilio wa homoni na hivo kuimarisha ubora wa tendo la ndoa.
- Mafuta ya rose yanaweza kutumika na pafyumu yako ya asili, ukaepuka kutumia pafyumu za viwandani zenye kemikali na sumu nyingi.
Jinsi ya kutumia Mafuta ya Rose
Mafuta haya yanafanya kazi vizuri endapo ukiweka kwenye diffuser ama ukapakaa kwenye ngozi. Kabla ya kutumia nashauri kuchanganya mafuta ya rose a mafuta mengine ili kupunguza makali, unaweza kuchanganya na mafuta ya bergamout, nazi, jojoba au mafuta ya tangawizi.
- Kwa msongo wa mawazo na wasiwasi kupita kiasi: changanya mafuta ya rose na mafuta ya lavender kisha weka kwenye diffuser. kama huna diffuser pakaa mchanganyiko huu kwenye maungio kiganja na mkono na nyuma ya shingo yako.
- Kuondoa chunusi: changanya mafuta ya rose na mafuta ya nazi kisha kwa kutumia oamba jipake kwenye uso wako mara mbili kwa siku.
- Kuimarisha hamu ya tendo la ndoa: Changanya mafuta ya rose a mafuta ya jojoba au olive kisa tumia diffuser au kama huna diffuser pakaa mchanganyiko huu kwenye kifua na na nyuma ya shingo
- Kwa maumivu wakati wa hedhi na dalili zingine mbaya siku chache kabla ya hedhi pamoja na dalili za kukoma hedhi: Changanya mmafuta ya rose na mafuta ya nazi kisha weka kwenye diffuser au fanya masaji kwenye tumbo.