Tiba ya Maumivu ya Viungo

arthritis

Maumivu ya joint ni tatizo linalosumbua watu wengi kwa sasa kutokana na mabadiliko ya mitindo ya Maisha. Umri mkubwa ni moja ya sababu inayopelekea kutokea kwa tatizo, ambapo tishu za mwili zinakuwa kavu na kupoteza uwezo wa kuvutika. Watu wengi wanafikiri kwamba kufanya mazoezi ni hatari kwa afya ya joints lakini ukweli ni kwamba ili kuepuka magonjwa ya joints mazoezi ni lazima katika kuongeza ufanisi wa viungo pia.
Nina uhakika kuwa umewaona akina mama wenye umri mkubwa na miili mikubwa wanavyopata shida kutembea huku wakiinama toka upande mmoja hadi mwingine kila wakipiga hatua au shida wanayopata pale inapowabidi kupanda ngazi au kukuchuchumaa. Maneno kama “ugonjwa wa kuumwa joints, nina tatizo la joints, maumivu ya joints” na maumivu ya mifupa umeyasikia mara nyingi. Tatizo hasa hapa ni nini? Ungana nami katika mada hii uujue ugonjwa huu wa arthritis lakini pia tiba ya mafuta asili ya eucalptus.

Ugonjwa wa Arthritis ni nini

Arthritis ni ugonjwa unaotokana na namna yoyote ya hitilafu katika maungio ya mifupa ya binadamu ambao husababisha maumivu na pengine kuvimba katika sehemu moja au zaidi ya maungio hayo. Neno arthritis halilengi ugonjwa mmoja bali jamii ya magonjwa ambayo kwa ujumla yapo zaidi ya 100. Tabia kuu ya magonjwa haya ni maumivu kwenye maungio ya mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo moja.

Chanzo cha Maumivu ya Viungo(Arthritis) ni nini

Kuelewa chanzo cha ugonjwa huu, hebu kwanza tutazame muundo wa joint au sehemu mifupa miwili inapokutana. Fikiria goti ambapo mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu vinapokutana:Ligaments: Ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja. Hii ni kama utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje, ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.
Cartilage: Huu ni utando unafunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja. Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.
Capsule: Hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote. Ndani ya mfuko huu wa capsule kuna synovial fluid ambayo huzalishwa na synovial membrane. Synovial fluid ni ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio kwenye kuta za ndani za capsule.
Ugonjwa wa arthritis unasababishwa na hitilafu yoyote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa. Inaweza kuwa cartilage inalika, upungufu wa synovial fluid, maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo.

Aina za Ugonjwa wa Arthritis(Maumivu ya Viungo)

  • Osteoarthritis: Hii ni aina ya arthritis inayosumbua watu wengi zaidi kuliko aina nyingine zote. Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa. Osteoarthritis hutokea pale cartilage inapopoteza uwezo wake wa kubonyea na kuwa ngumu hivyo kuharibika haraka. Cartilage ni kiungo cha kuhimili migandamizo ya ghafla (shock absorber). Cartilage hii inapopoteza ubora wake, tendons na ligaments huvutika na kusababisha maumivu. Hali ya uharibifu huu wa cartilage ikiendelea, mwishowe mifupa huanza kusuguana moja kwa moja na ndipo mgonjwa atakapoanza kupata maumivu makali sana.
  • Rheumatid Arthritis: Ugonjwa huu hutokea pale mfumo wa kinga ya mwili kwa bahati mbaya kuanza kushambulia viungo vya mwili ikiwa ni pamoja na synovial membrane (synovium) na kusababisha uvimbe na maumivu. Hali hii isipodhibitiwa, huweza kusababisha ulemavu. Ugonjwa huu unaweza pia kushambulia macho, ngozi, mapafu, midomo, damu na mishipa ya damu
  • infectious Arthritis (Septic Arthritis): Aina hii ya arthritis inatokana na maambukizi ya bacteria kwenye synovial fluid. Maambukizi haya yanaweza kuwa pia ni ya fungus au virusi. Wadudu kutoka sehemu nyingine ya mwili iliyo karibu na maungio ya mifupa huweza kusambaa kupitia mfumo wa damu hadi kwenye joint na kuleta maambukizi.

Tiba Kupitia Mafuta ya Eucalyptus

mafyta ya mkaratusi
mafuta ya eucalyptus

Mafuta ya eucalptus yamekuwa yakitumika kwa zaidi ya miaka 2000 kutibu maumivu na kupunguza kuvimba kwa mwili, kwa miaka ya sasa mafuta haya yamegundulika kuwa na uwezo mkubwa zaidi na kutibu changamoto nyingi:
Kutibu maumivu ya misuli na joints: chovya kiasi kidogo cha mafuta haya kwa kutumia pamba au kitambaa laini kisha sugua eneo lenye maumivu mara mbili kwa siku. Tunashauri mgonjwa atumie walau dozi mbili za dawa.
Huhitaji tena kuagiza nje ya nchi, tayari tumefanya utafiti wa mafuta salama yasiyochakachuliwa na kukuletea hapa. Wasiliana nasi ufike ofsini kwetu ama tukutumie ukiwa mkoani.

Chati nasi whatsapp kwa namba 0746672914 kupata mafuta original ya Eucalyptus kwa Tsh 40,000/= tu