Maumivu kwenye sikio na kutoa Usaha

maumivu kwenye sikio

Maumivu kwenye sikio ni ya kawaida sana na yanawatokea watu wengi hasa kwa watoto. Maambukizi hasa yanasababishwa na bakteria na yanaweza kupeleka masikio kutoa uchafu mwingi na usaha. Maambukizi haya hutokea kwenye eneo la kati sikio kwa ndani ambalo liko nyuma ya ngoma ya sikio. Endapo bomba ya kutirisha uchafu litaziba, maji yatakusanyika kwenye sikio la kati na kusababisha maambukizi. Bomba hili huitwa Eustachian tube na linaweza kuziba kutokana na mafua na maambukizi ya pua, ute mzito zaidi, aleji kutokana na moshi.

Majira yapi unaweza kupata maumivu kwenye sikio?

Maambukizi ya sikio yanatokea zaidi wakati wa majira ya baridi ambapo watoto wanaweza kupata mafua kirahisi. Dalili za kuonesha kuna shida kwenye sikio ni pamoja na kujaa maji nyuma ya utando wa sikio ambayo husababisha maumivu na kuwashwa, hisia ya kufunga sikio, na kupoteza kusikia katika sikio lililoathiriwa. Ikiwa utando wa sikio utapasuka, basi kutokea kutokwa na usaha mweusi kutoka sikioni.

Tiba mbadala ya maumivu kwenye sikio

1.Tangawizi

tangawizi

Tangawizi ina vimabata tiba vyenye nguvu ambayo hutumiwa sana kutibu na kuponya magonjwa na matatizo mbalimbali.

Ni mojawapo ya njia bora za kutibu aina zote za maambukizi kutokana na uwezo wake wa kuzuia bakteria, kupambana na viini na kupunguza kuvimba kwa tishu laini za ndani. Kata tangawizi safi na uchuje juisi yake. Tia matone machache ya juisi hii ndani ya sikio linalouma mara tatu kwa siku.

2.Kitunguu Saumu kutibu maumivu kwenye masikio na usaha

Kitunguu saumu ni njia nyingine ya asili ambayo itaponya maambukizi kwa haraka na kwa ufanisi. Ina viambata vyenye nguvu ya kupunguza kuvimba kwa ndani na maumivu pia. Matumizi: Pasha mafuta ya mzeituni na kaanga kitunguu saumu ndani yake kilichokatwakatwa kwenye mafuta. Yaache mafuta yapoe kwa saa 1 au mawili kisha tia matone machache ya mafuta kwenye kwenye njia ya sikio.

3.Mafuta ya Haradali

Mafuta ya haradali ni dawa ya mda mrefu kwa maumivu katika mwili. Uwezo wake wa kusafisha, kupunguza uvimbe, na kupambana na bakteria itaondoa maambukizi kwa mafanikio na kusaidia kuponya sikio lako kwa haraka.
Pia mafuta ya haradali yasaidia kukausha maji machafu yaliyokusanyika ndani ya sikio na kuleta nafuu mapema. Matumizi: Pasha mafuta ya haradali kwa mbali sana kwa kuweka kwenye bakuli la chuma juu ya maji ya moto. Tia matone machache ndani ya masikio yako na upumzike.Hakikisha unatia matone ya mafuta mara mbili au tatu kwa siku kwa siku 5 ili upone kabisa.