Mafuta ya Rose ni Tiba kwa Maumivu ya Tumbo la hedhi.

mafuta ya rose
mafuta ya rose

Kitabibu kwa maumivu kipindi cha hedhi hutokana na kusinyaa na kutanuka kwa misuli ya mji wa mimba wakati wa kipindi cha hedhi ili kuruhusu kumeguka kwa ukuta wa mfuko wa mimba na kutoa damu iliyochanganyika na yai ambalo halikurutubishwa nje. Mumivu haya yamegawanyika katika aina mbili.

Maumivu Ya Hedhi Aina Ya Kwanza Ya Kawaida (Primary)

Maumivu haya ni ya kawaida kabisa kwa wanawake wanapopitia kipindi hiki ambacho hujirudia kila mwezi. Maumivu kikawaida huanza kati ya siku moja ama mbili kabla ya hedhi kuanza kutoka, mwanamke hujiskia mamumivu haya kwenye tumbo la chini na kwenye nyonga na kiuno kwa ujumla. Maumivu yanaweza kuwa madogo au yakawa makali sana na huisha ndani ya masaa 12 mpaka 72 huku yanaweza kuambatana na kutapika na kupata kizunguzungu. Kwa wanawake wengi maumivu haya ambayo ni ya kawaida kabisa hupungua kadiri umri unavoenda na pia pale mwanamke kijifungua.

 Maumivu Aina Ya Pili Yasiyo Ya Kawaida(Secondary)

Maumivu haya ni kutokana na tatizo fulani la kiafya kweye via vya uzazi vya mwanamke kama vile uvimbe usiyo wa saratani ndani ya mfuko wa mimba, kukua kwa tishu laini za mfuko wa mimba kuelekea kwenye viungo vingine kama uke na mifuko ya mayai na pia kupanuka kwa ukuta wa kizazi kutokana na kukua kwa tishu za ndani kuelekea ukuta wa nje.

Maumivu haya pia yasiyo ya kawaida yanaweza kuwa yamesababishwa na athari za bakteria ama virusi katika via vya uzazi. Kikawaida maumivu haya huanza mapema zaidi wakati wa hedhi naa huchukua muda mrefu zaidi kuisha ukilinganisha na maumivu yake ya kawaida na pia maumivu haya yanakuwa hayaambatani na kutapika, kuharisha, kizunguzungu wala kukosa nguvu na ganzi. Kwa aina hii ya maumivu ni muhimu ufike mapema hospitali ufanyiwe vipimo kugundua chanzo cha tatizo lako uanze kutibua ugonjwa husika mapema.

Lini unatakiwa Kumwona Daktari kwa ajili ya vipimo?

Kama maumivu yako  ni makali zaidi kuliko kawaida na yanachukua zaidi ya siku 3 hakikisha unamwona dactari wako haraka, kwanini? kwasababu yawezekana maumivu yako siyo ya kawaida na yaweza kuwa una uvimbe ama maambukizi ya bacteria na virusi kwenye mfuko wa mimba, hivo kuwahi hospitali itasaidia kutibu tatizo lako mapema kabla halijawa kubwa. Pia tunashauri kuwahi kumwona dactari kwa sababu ukuaji wa tishu za mfuko wa mimba unahusishwa na kusababisha saratani ya shingo ya kizazi, na hivo kujua chanzo cha tatizo lako mapema kutasaidia kulitibu mapema.

Ufanye nini ili Unapopata Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi?

  • Meza dawa za kukata maumivu kwa ahueni ya haraka. Angalizo: dawa za maumivu isiwe ni nia ya kutumika kila mara kwani madhara yake ni makubwa kiafya, dawa hizi zitumike kwa uangalifu.
  • Tumia maji ya uvuguvugu kukandakanda mahali pa tumbo la chini ukiwa umelala chali
  • Usitumie vinywaji na vyakula vyenye caffeine mfano majani ya chai, chokoleti na kahawa
  • Fanya masaji kwenye upande wa chini wa mgongo na sehemu ya tumbo la chini
  • Pata muda mwingi wa kupumzika na
  • Weka ratiba ya kufanya mazoezi mara kwa mara, tafiti zinasema wanawake wanaofanya mazoezi hupunguza maumivu ya hedhi kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na wasiofanya mazoezi.

Tiba Muhimu na Asili Maumivu kipindi cha Hedhi kupitia Mafuta ya Rose.

Mafuta ya rose hupatikana kutoka na maua ya mmea wa Rose. Miti yake yenye miiba yake inaweza kukua kwa kujitegemea ama ikakua kwa kujizungusha kwenye mti mwingine.
Mafuta ya Rose ni tiba nzuri, asili na salama kupunguza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi na pia kupunguza dalili mbaya kwa mwanamke aliyekoma hedhi kama kukosa hamu ya tendo na uchovu mwingi.

Jinsi ya Kutumia mafuta ya Rose

Kwa maumivu wakati wa hedhi na dalili zingine mbaya siku chache kabla ya hedhi : Chovya kiasi kidogo cha mafuta ya Rose kwa kutumia pamba au kidole kisha fanya masaji kwenye tumbo kwa muda wa dakika 10 mpaka 15 fanya hivo kwa siku zote za hedhi. Rudia matumizi ya mafuta kwa miezi miwili inayofuata kipindi cha hedhi.

Kwa mwanamke aliyekoma hedhi na anakosa hamu ya tendo: Fanya masaji ya eneo la tumbo na mgongo kupitia mafuta haya mara 3 kwa week.

Muhimu kufahamu

Kuna tofauti kati ya mafuta ya rose,rose water, mafuta ya rosemary na mafuta ya primrose. Mafuta mengi ya rose yaliyopo mtaani hayana ubora unaotakiwa na ndiomaana tumejitahidi kufanya utafiti na kukuletea mafuta yetu asili ya Rose yasiyochakachukuliwa kwa kuendana na thamani ya pesa yako ili ufurahie faida zake.

Chati nasi whatsapp kwa namba 0746672914 kupata mafuta original ya rose kwa Tsh 40,000/= tu