Njia 5 za Asili Kutibu Maumivu ya Meno

Maumivu ya meno yanaweza kutufanya tulie, kuteseka na kukosa amani. Wale ambao tumekumbana na maumivu ya meno tunajua kuwa si jambo la kucheka. Maumivu yanayohusiana na jino yanaweza kusambaa hadi kwenye fizi na taya pia.

Kwa kawaida, maumivu yanayohusiana na jino yanatokana na aina fulani ya hitilafu kwenye meno na maeneo yanayozunguka. Baadhi ya sababu za kawaida zinazosababisha maumivu ya jino ni uvimbe, nyufa kwenye meno, magonjwa yanayohusiana na fizi, kuoza kwa meno n.k.

Muhhimu kujitayaraisha juu ya maumivu ya meno

Kwa kuwa maumivu ya meno hayawezi kutabiriwa na yanaweza kutokea wakati wowote wa siku, ni wazo zuri kuwa tayari na njia za asili badala ya kukimbilia hospital kila mara. Njia za asili za kutibu maumivu ya meno ni faraja kubwa kwa wale waumini wa tiba mbadala zisizo na sumu. Maumivu ya meno wakati wa ujauzito lazima yatibiwe kwa umakini maalum kwani bakteria katika meno yaliyoathiriwa yanaweza kuingia kwenye mzunguko wa damu ya mama na kusababisha madhara kwa mtoto. Kwa wengine ambao wanakabiliwa na maumivu ya meno ya wastani, njia za asili ni muhimu sana.

1.Kitunguu Saumu

Kutokana na uwezo wake wa kupambana na bakteria yani(antbiotics) kwenye kitunguu saumu, matatizo ya maumivu ya meno hupata nafuu kwa kutumia kitunguu saumu.

Matumizi: Chukua kitunguu saumu punje mbili, zipondeponde kisha weka chumvi ya mawe pamoja na kitunguu saumu kwenye jino lililoathiriwa. Hii ndiyo inayohitajika ili kupunguza maumivu. Huenda ukashangazwa kuwa kinaweza hata kutibu maumivu ya meno ya wastani kikamilifu. Kiambata cha allicin kilichopo kwenye kitunguu saumu ndicho kinachotoa tiba hii ya ajabu. Allicin hutoa matokeo sawasawa na dawa za kuua bakteria na ni antbiotics ya asili. Hata hivyo, inaweza kuwa nafuu ya muda, labda itakusaidia kupita usiku. Hakikisha unapanga kumtembelea daktari ikiwa tatizo litaendelea.

2.Kitunguu Maji kutibu maumivu ya meno

Kama kitunguu saumu, kitunguu maji pia kina uwezo wa kuua bakteria(antibiotics). Unachohitaji kufanya kila siku ni kutafuna kitunguu maji kwa dakika chache. Hii itaondoa bakteria wabaya karibu wote kinywani na kuzuia shida nyingi zinazohusiana na meno. Kwa maumivu ya meno, kata vipande kadhaa vya kitunguu maji na viweke kwenye jino lililoathiriwa. Ili kuepuka maumivu ya meno, hakikisha unatafuna kitunguu maji kila siku au uviweke kwenye mlo wako kama saladi.

3.Ndimu ni tiba ya maumivu ya meno

ndimu kutibu maumivu ya meno

Vitamini C iliyopo kwenye ndimu husaidia kupambana na maambukizi kwa ujumla. Vitamini C pia ni kiungo kizuri linapokuja suala la afya ya meno na mifupa. Pia vitamini C inazuia kuoza kwa meno na magonjwa mengine ya fizi. Kwa kupunguza maumivu ya meno, chukua ndimu na uikamue. Iweke katika uwazo wa jino. Ndimu ina viwango vya juu vya vitamini C na viwango vya chini vya asidi ikilinganishwa na limau na ndio tiba bora kuliko limau kwa maumivu ya meno.

4.Karafuu

karafuu

Karafuu zimetumika kwa vizazi na vizazi kwa ajili ya kutibu maumivu ya meno. Mara moja inatoa hisia ya utulivu ndani ya kinywa na kuzuia hisia ya maumivu. Karafuu ni dawa za kuua bakteria ya asili na hivyo kuweka karafuu kwenye jino sio tu inatuliza maumivu ya meno lakini pia itaua bakteria ambao wamesababisha maumivu hayo. Unaweza kutumia karafuu au mafuta ya karafuu kwa kuweka kwenye jino linalouma.

5.Peppermint-mnanaa

Wakati unapopata maumivu ya meno ambayo yanazidi, nenda haraka jikoni na uandae mchanganyiko wa mnana na chumvi ya kawaida na bila kupoteza muda, weka kwenye jino linalokupa maumivu ya kuteseka. Subiri kwa sekunde chache na uone maajabu ya mchanganyiko huu. Mnanaa pamoja na chumvi inaitwa pia inafaa kuzuia harufu mbaya ya kinywa, maumivu na kutokwa damu kwa fizi, mashimo na bila shaka maumivu ya meno. Kama unakosa mnanaa basi agiza mafuta original ya mnanaa kutoka kwetu ili uanze tiba mapema.