Tiba ya Tonses Sugu

tonses sugu

Njia za Asili za kutibu Kuvimba Tonses sugu

Tonses inatokana na neno tonsil ambazo ni tezi zilizopo nyuma ya mdomo, kazi yake ni kuchuja bakteria wabaya na vimelea mdomoni. Lakini tezi hizi zinaweza kupata maambukizi ambapo zinapaswa kupigana na kuyatoa mwilini. Hivyo, zina jukumu muhimu katika mfumo wetu wa kinga. Maambukizi yanapojirudia mara kwa mara ndio tunaita tonses sugu na hapo unahitaji tiba asili za mimea kupona.

Zinajaribu kuzuia kuingia kwa bakteria na virusi mwilini. Umbo lao linafanana na la kishubaka, na zipo nyuma ya kinywa, moja upande wa kulia na moja upande wa kushoto. Endapo unaugua tonses mara kwa mara, unapaswa kuanza kutumia njia za asili mara moja na kuzuia hali isiendelee kuwa mbaya.

Nini kinafanya uugue tonses sugu

Maambukizi ya bakteria au virusi ndio sababu za tonses. Bakteria wanaosababisha koo kuuma wanaweza kuwashambulia tonsili na kuleta maambukizi. Mzio au aleji inaweza kusababisha tonses kuvimba .Vyakula baridi kama barafu na vinywaji baridi sana havifai kwa baadhi ya watu na ndivyo sababu kuu ya kuvimba tonses kwa watu kama hao.

Kando na barafu, vyakula vingi vinavyochemsha na vyenye pilipili kali vinaweza kusababisha tonses. Kupungua ghafla kwa joto kunaweza kusababisha tonsiliti kwa watu kama hao, kwani linapunguza kiwango cha kinga.

Tiba mbadala za Tonses sugu

1.Kusukutua kwa maji ye chunvi

Hakuna kitu kinachofanya kazi vizuri kama maji ya moto yenye chumvi kwa tonsili. Hata hivyo, punguza kiasi cha chumvi au achana nayo kabisa ikiwa maambukizo ni makali. Katika kesi hiyo, chumvi itachoma tonsili zilizovimba na kuzidisha hali. Weka robo kijiko cha chumvi kwenye glasi kamili ya maji ya moto. Kama utafuata njia sahihi ya matumizi , itakusaidia sana. Joto la maji ya chunvi linapaswa kuwa la kutosha ili uweze kulivumilia. Kunywa kidogo na nyanyua kichwa chako kana kwamba unatazama dari na fanya kuyazungusha maji kwenye koo kisha yateme .Fanya hivo mara 8 hadi 10 kila siku.

2.Tumia Barafu kufunika

Barafu mara nyingi husaidia kupunguza uvimbe wa tonsili. Wakati uvimbe unapungua, maumivu pia hupungua. Ili kutengeneza barafu ya kufunika, chukua tonge moja kamili ya barafu, weka kwenye mfuko usioingiza maji. Sasa weka kifuani kwa dakika 15 . Utashuhudia dalili za tonses zinapungua.

3.Unga wa manjano

Unga wa manjano ni unga wenye nguvu wa asili unaotokana na mizizi ya mmea. Hakikisha unatumia unga safi na mpya wa manjano. Kemikali inayoitwa curcumin iliyo ndani yake ina nguvu ya kutibu. Matumizi: Weka kiwango kidogo cha unga wa manjano kwenye kikombe cha maziwa na chemsha, endelea kwa dakika 5. Unaweza kuongeza asali na kunywa kila usiku kabla ya kwenda kulala.

4.Ndimu

Kinywaji kilichotengenezwa kwa kutumia juisi ya ndimu na asali ni bora kwa tonsili zako. Juisi ya ndimu inakupa vitamini C ambayo inakuwa muhimu kuponya tonsili zilizoathiriwa. Asali inajulikana kwa matokeo yake ya kutuliza koo. Asali hutoa kinga koo na kupunguza kuvimba.

5.Unga au Mbegu za uwatu

Matumizi: Loweka vijiko 2 vya mbegu za uwatu usiku kucha. Kisha chemsha kwa dakika 5. Kiasi hiki kinatosha kwa matumizi ya siku moja. Unaweza kutengeneza glasi 2 na uwatu angalau mara 5 kila siku. Inajulikana kuwa uwatu unapunguza uvimbe na maumivu kwenye tonses.