Tiba asili ya fizi kuvuja damu na meno kutoboka

fizi kuvuja damu

Tiba za Nyumbani kwa Fizi Kuvuja damu

Fizi kuvuja damu ni hali inayotokea kutokana na maambukizi ya vimelea mbalimbali kwenye eneo tishu laini zinazoshikilia meno yako yaani fizi. Pia usafi duni wa kinywa inaweza kusababisha fizi zako kuwa hatarini. Kuvuja damu kwenye fizi kwa kawaida hutokea wakati wa kusafisha meno au unapotafuna matunda mbichi yenye ugumu.

Tiba rahisi za nyumbani ni za ufanisi sana katika kutibu kuvuja damu kwenye fizi katika hatua za awali.
Pamoja na tiba za nyumbani, unapaswa kumtembelea daktari wa meno mara moja kila miezi sita ili kusafisha vizuri na kuondoa uchafu wa fizi ili kuzuia magonjwa ya fizi na matatizo ya meno kama vile meno kutoboka na kuoza.

Tiba Mbadala za Nyumbani kwa Fizi kuvuja damu.

1.Kusukutua kwa Chumvi ya Maji

Chukua glasi moja ya maji ya uvuguvugu na weka nusu kijiko cha chai cha chumvi ya kawaida. Tumia maji haya kwa kusukutua baada ya kusafisha meno. Husaidia kuondoa uvimbe na maumivu kwenye fizi zinazovuja damu.

2.Kusukutua kwa Limau

Limau lina kiwango kikubwa cha vitamini C na husaidia kuimarisha fizi zenye afya. Kata nusu ya limau na kamulia kwenye glasi moja ya maji na itumie kusukutua kinywa baada ya mlo. Fanya hili zoezi asbhi na jioni kwa wiki moja

3.Fanya masaji ya fizi zako

Kumasaji fizi ni muhimu sana kwa kudumisha fizi zenye afya. Husaidia kuzuia kuvuja damu kwenye fizi na pia husaidia kutibu. Sukutua fizi mara mbili kwa siku baada ya kusafisha meno. Tumia kidole cha shahada na kidole gumba kumasaji fizi taratibu.

4.Matunda kutibu fizi kuvuja damu

Kudumisha usafi wa mdomo, unapaswa kula vyakula vyenye manufaa kwa afya ya meno yako. Matunda yenye uchachu yani citrus frits yana kiwango kikubwa cha vitamini C. Ni muhimu sana kwa ajili ya fizi zenye afya. Chukua machungwa, limau, brokoli, kabichi, ndimu, na nanasi n.k. vyenye kiwango kikubwa cha vitamini C.

Kula angalau chakula kimoja chenye kiwango kikubwa cha vitamini C kila siku ili kutibu kuvuja damu kwenye fizi. Maziwa ni muhimu kwa kudumisha meno na fizi zenye afya kwani yanayo kalsiamu na protini pamoja na vitamini muhimu. Kunywa angalau glass moja ya maziwa kila siku ili kutibu kuvuja damu kwenye fizi.

5.Juisi ya mbogamboga

Kusaga mboga mboga mbichi ni tabia njema kwa afya. Inaimarisha fizi na hata mfumo wa chakula. Chukua karoti, au kabichi na kusaga kwa dakika 1-2, chja kisha weka na lima kuongeza ladha. Tumia juisi ya mbogamboga mara 4 kwa wiki.