Hatua 6 za kuacha ulevi wa Pombe

Tiba za Nyumbani za Kupambana na Ulevi wa Pombe

Ulevi wa pombe umekuwa sehemu ya maisha kwa watu wengi sana kwa miongo na karne. Tunaposema ulevi wa pombe sio tu matumizi ya pombe, bali ni yale matumizi mabaya ya pombe kupita kiasi. Wakati unapokunywa pombe nyingi muda mrefu, mwili unakuwa na utumwa zaidi kwa pombe na pia unakuwa tegemezi zaidi kwa pombe.

Zifuatazo ni njia salama unazoweza kufatilia ukiwa nyumbani kwako, endapo una nia ya dhai kabisa kuachana na ulevi wa pombe.

1.Tufaha kwa Tiba ya Ulevi wa Pombe

tufaa kuondoa ulevi wa pombe

Tufaha au apple ni chanzo kizuri cha virutubishi na ni nzuri kwa afya ya mwili. Hasa, tufaha zinafahamika kwa uwezo wake wa kuondoa sumu zilizojilundika ndani ya mwili. Na tufaha husaidia hasa ini na kusaidia katika kusafisha ini ambalo linaweza kuathiriwa na madhara ya pombe.

Hii ni tiba nzuri yenye ufanisi ya nyumbani kwkao kuondoa ulevi wa pombe. Juisi ya tufaha ina kiwango kikubwa cha asidi ya malic(malic acid), acid ambayo ni kiungo muhimu katika vyakula vyenye ladha ya uchachu, kama vile matunda ambayo hayajakomaa. Asidi ya malic inajulikana kuwa na matokeo mazuri kwenye ini na ngozi, kwani ina uwezekano wa kupunguza madhara ya sumu kwa kuondoa sumu zilizojilundika kwenye mwili.

Watu waliopo kwenye programu ya kuacha matumizi ya pombe kutoka wanahimizwa kula tufaha kadhaa iwezekanavyo katika siku za kwanza, ili kusaidia kusafisha kwa ufanisi na kurejesha seli za ini zilizoharibiwa na pombe.

2.Tende kwa Tiba ya Ulevi wa Pombe

Chaguo lingine la tiba ya ulevi wa pombe ni tende. Imegundulika kuwa tende zinasaidia kupunguza hamu ya pombe na kusaidia kushinda tamaa ya kunywa pombe wakati wa kupona kutoka kwa ulevi wa pombe. Njia rahisi ya kutumia njia hii ni kwa kuzisaga tende kwenye blender na kuchanganya katika maji ili kutengeneza juisi. Tumia juisi hii mara mbili kwa siku kwa muda wa mwezi mmoja, ili ujione mabadiliko ya ajabu katika hamu ya pombe.

Zaidi ya hayo, tende zina mchanganyiko mkubwa wa madini na vitamini muhimu, kama vile calcium , potasiamu, fosforasi, manganisi, magnesiamu, na shaba, ambazo ni muhimu kwa kupona na kuboresha afya kutokana na ulevi wa pombe.

3.Juisi ya Karoti

juisi ya karoti

Ukipata kiu ya ama hamu ya ghafla kunywa pombe, wazo zuri ni kunywa juisi ya karoti. Tafiti zimeonesha kwamba juisi ya karoti inapunguza hamu ya kunywa pombe kwa walevi wakati wa kipindi cha kupona. Na pia ni chanzo kizuri cha vitamini na madini mengi. Bila shaka, utapata faida nyingine nyingi pia unapobadilisha pombe na juisi ya karoti kwa wakati unaofaa.

4.Juisi ya Ndimu

Unaweza kutaka kunywa juisi ya ndimu na chumvi na sukari unapohisi hamu ya kunywa pombe. Utapenda ladha yake nzuri na ladha yake ya kutuliza, ambayo itakuwa yenye kuvutia peke yake wakati inakufanya usifikirie kuhusu pombe. Maandalizi yake ni kwa kukadiria tu kiwango flani cha sukari, chunvi kiasi na ndimu 3 kwa maji glass moja.

5.Juisi ya Machungwa

Hali ni kama ilivyo kwa juisi ya ndimu, ambayo ni tiba ya nyumbani yenye ufanisi kwa ulevi wa pombe. Chungwa ni tunda lenye asidi na lina ladha ya kusisimua, huku harufu yake ikikuvutia na kukata tamaa yako ya pombe. Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya limau na juisi ya machungwa kila siku ili kuhakikisha unajiepusha na ulevi wa pombe.

6.Punguza Sukari kama Tiba ya Ulevi wa Pombe

Kuna na uhusiano fulani kati ya ulevi wa sukari na tamaa ya pombe. Ikiwa unaweza kupunguza ulaji wa vyakula na vinywaji vya sukari , huenda ukaona hamu ndogo ya kunywa pombe. Kupunguza ulaji wa sukari pia husaidia kudumisha afya nzuri.

Badala ya kula sana vyakula vya sukari, anza kwa kuweka kwa wingi vyakula vyenye mafuta mazuri kama parachichi, mbegu za maboga, ufuta, mafuta ya olive, chia seed, samaki na mafuta ya nazi.

Angalizo

Endapo umeshaanza tiba ya hospitali usikatishe njiani. Lengo letu siyo kukufanya uache matibabu ya daktari wako. Lengo letu ni kukusaidia upate nafuu wakati unajiandaa kwenda hospitali. Kama njia zote hizi hazijakupa matokeo mazuri, tafadhali nenda hospital mapema muone daktari. Yawezekana kuna tatizo kubwa kiafya linalohitaji uangalizi wa karibu na vipimo zaidi.