Tiba ya kikohozi sugu bila kumeza dawa

Kikohozi ni hali ambayo inakumba mtu mara kwa mara. Watu wa umri wote hupata kikohozi kutokana na sababu mbalimbali. Badala ya kutumia dawa za dukani za kikohozi, unaweza kujaribu moja ya Tiba za asili kwa Kikohozi sugu, tiba hizi ni salama na zenye ufanisi. Tiba za nyumbani kwa kikohozi hazisababishi athari yoyote, isipokuwa kama una aleji kwa kiungo fulani ndipo unatakiwa kutumia kwa uangalifu.

1.Asali na Tangawizi

Asali ni kinga dhidi ya sumu kwenye mwili, pia inaaleta matokeo kwenye kupambana na maambikizi ya bakteria. Asali ina matokeo mazuri kwenye ya kutuliza koo na hutoa nafuu ya haraka kutokana na kikohozi kikavu. Tangawizi pia inasaidia kupambana na bakteria wabaya. Pia tangawizi hujenga kinga yako dhidi ya mzio/aleji ya kawaida. Tangawizi inakuwa ni tiba yenye nguvu ya nyumbani kwa kikohozi unapochanganya na asali.

Matumizi: Chukua kipande kidogo cha tangawizi, osha kisha twanga au saga kwenye blender. Chukua sufuria weka maji kidogo na tangawizi iliyosagwa chemsha dakika 5. Epua na weke asali kwenye chai yako na unywe mara tatu kwa siku. Usile au kunywa kitu chochote mara moja baada ya kunywa mchanganyiko huu mpaka nusu saa ipite.

2.Limau kutibu kikohozi sugu

Limau lina kiasi kikubwa cha Vitamini C, ambayo inaimarisha mfumo wako wa kinga na husaidia kulinda dhidi ya aina mbalimbali za maambukizi. Limau na asali ni tiba yenye ufanisi ya nyumbani kwa kikohozi sgu, pia mcganganyiko huu unasaidia usingizi mzuri baada ya kunywa kabla ya kulala. Chukua kijiko kimoja cha juisi ya limau, ongeza kijiko kimoja cha asali na nusu kikombe cha maji ya uvuguvugu. Kunywa taratibu ili kupunguza makali ya kikohozi.

3.Manjano (tumeric)

Manjano ni dawa ya asili ya kuua vijidudu na bakteria. Mara nyingi hutumiwa zaidi na wadada kusafisha uso na kuongeza urembo. Manjano inasaidia kutuliza koo na kutoa nafuu ya kikohozi. Chukua robo kijiko cha chai ya unga wa manjano, ongeza kijiko kimoja cha asali. Kula mara mbili kwa siku dakika 30 baada ya mlo ili kupunguza kikohozi. Tiba hii inaweza kuendelezwa kwa muda mrefu kutibu kikohozi sugu.

4.Maziwa na Manjano

Chukua glasi moja ya maziwa ya uvuguvugu, ongeza robo kijiko cha chai ya unga wa manjano na kunywa taratibu ili kupunguza kikohozi. Maziwa husaidia kutoa nishati na nguvu ambazo mara nyingi hupungua baada ya kikohozi cha mara kwa mara. Tumia mchanganyiko huu wakati wa kulala ili kupata usingizi mzuri. Hii ni muhimu hasa wakati wa baridi. Manjano daima inapaswa kutumiwa kwa kiasi kidogo.

5.Mlozi(Almond)

almond kutibu kikohozi sugu

Mlozi una lishe kubwa. Una kalsiamu, chuma, fosforasi, magnesiamu, vitamini E, zinki, shaba n.k. Unasaidia kutibu kikohozi kikavu na kisichoisha. Loweka lozi kiganja kimoja na maji nusu lita kwa usiku kchaku, asubuhi yake unaondoa ganda na kusaga kwa blender ili kupata uji mzito. Ongeza kijiko kimoja cha unga wa manjano na kula kwenye tumbo tupu. Endelea kutumia tiba hii kwa siku 15 kutibu kikohozi cha muda mrefu. Tiba hii itasaidia kutoa makohozi kwa urahisi.

6.Mafuta ya mustard (haradali)

mafuta ya haradali

Mafuta ya haradali yana historia kubwa sana kwenye uponyaji. Hutumiwa kupikia na pia kwa kupaka kichwa na mwili. Mafuta ya haradali hupenya ndani ya ngozi na husaidia kutuliza aina mbalimbali za maradhi.

Kutibu kikohozi sugu, pasha mafuta ya haradali na yapake mgongoni na kifuani wakati wa kulala. Itasaidia kuondoa mkusanyiko wa makohozi kifuani na kukusaidia kupumua kwa urahisi. Paka mafuta ya haradali ya uvuguvugu kwenye unyayo wa mguu wako wakati wa kulala na funika miguu na soksi za pamba. Utapata usiku mzuri bila kikohozi kinachosumbua usingizi wako. Tiba hii hufanya maajabu sana hata kwa watoto wadogo.