Mbinu 5 za Kundoa Weusi kwenye kwapa

weusi kwenye kwapa

Weusi kwenye kwapa mara nyingi huwa inakufanya ukose uhuru wa kujiachia mbele za watu hasa kwa wanawake. Japo mtaani kuna bidhaa maarufu na nyingi sana zinatangazwa kumaliza tatizo, ukweli ni kwamba wanataka tu pesa yako.

Mafuta na dawa nyingi mtaani hazileti matokeo, kwa ujumla hazifanyi kazi vizuri. Weusi kwenye kwapa huwafanya watu wajitambue wanapovaa vazi la kuogelea au mavazi yasiyofunika mikono.

Nini kinasababisha weusi kwenye kwapa?

Weusi kwenye kwapa unasababishwa na vitu vingi ikiwemo

  • Kuwepo kwa seli zilizokufa
  • kutoka jasho kwa wingi,
  • kutumia kemikali za kuondoa nywele, kunyoa,
  • kutumia manukato na manukato yenye viambata vya pombe ni sababu za kfanya kuwa na kwapa nyesi kuwa nyeusi.

Unaweza kumaliza tatizo hili kwa kutumia tiba mbadala ya nyumbani, ambayo ni salama, asilia, na yenye ufanisi mkubwa.

Mbadala wa Nyumbani kusafisha weusi kwenye kwapa

1.Limau

Mbali na kuwa kisafishaji cha asilia, limaa pia ina uwezo wa kuua bakteria na vimelea wengine. Hivyo, hutumika kutibu matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwa ni pamoja na kwapa nyeusi. Sugua kipande cha limau kwenye eneo linaloathiriwa ili kuondoa seli zilizokufa na kuboresha mwonekano wa ngozi. Osha eneo hilo kikamilifu baada ya nusu saa kwa kutumia majiya uvuguvugu. Pia ni muhimu kutumia mafuta asili ya nazi kwenye eneo linaloathiriwa baada ya kusugua kwa limau, kwani juisi ya limau inaweza kusababisha ngozi kuwa kavu.

2.Siki (vinegar) kuondoa weusi kwenye kwapa

Changanya siki yaani vinegar yenye manjano na koroga kutengeneza uji mzito. Tia mkorogo huu kwenye eneo linaloathiriwa la kwapa baada ya kuoga. Acha mchanganyiko huu kwa muda wa dakika 10 – 15 na osha kwa maji ya uvuguvugu. Mbali na kuboresha rangi ya ngozi, mbinu hii pia itasaidia kuua bakteria na vijidudu vinavyosababisha harufu mbaya chini ya kwapa. Hakikisha unatumia apple cider vinegar.

3.Kuosha kwapa kwa Baking Soda

baking soda

Kuosha kwapa yako kwa kawaida kutasaidia kuiboresha rangi ya ngozi. Unaweza kuchanganya baking soda na maji. Osha kwapa yako kwa kutumia mchanganyiko huu na itasaidia kuondoa seli za ngozi zilizokufa zilizo kwenye eneo hilo. Hii pia ni moja ya sababu kuu za kiganja kuwa nyeusi. Kuosha huku kutasaidia kufungua nyufa za ngozi pia.

4.Ganda la chungwa

Maganda ya chungwa yana ufanisi mkubwa sana katika kuiboresha rangi ya ngozi. Kwanga maganda ya machingwa, kisha yakaushe kwa jua kwa siku chache. Kaanga na kusaga maganda yaliyokaushwa na kuhifadhi kwenye chombo. Tumia wakati wowote unapohitaji baada ya kuoga. Changanya maganda yaliyosagwa ya ukwaju, maziwa, na maji ya waridi ili kutengeneza rojo yenye kusokota. Tumia hii kupaka kwapa kwa muda wa dakika 10 – 15. Hatimaye, osha kwa maji. Hii itaondoa seli zilizokufa za ngozi.

5.Mafuta ya lavender kuondoa weusi kwenye kwapa

lavender oil

Mafuta ya lavender yanazalishwa zaidi nchi za Asia kama pakistani na india. Ni mafuta yenye umaarufu mkubwa sana duniani kwenye tasnia ya urembo. Hakikisha unanua mafta haya kwenye chanzo cha kuaminika ili uyapate yale original.

Matumizi: kuondoa weusi kwenye kwapa na hata kwenye mapaja, paka kiasi kidogo cha mafuta ya levender na mafuta ya nazi. Tumia mchanganyiko huu asubuhi na jioni baada ya kuoga kwa mwezi mmoja na utaona matokeo makubwa.