Tiba asili Kuondoa Makovu ya Chunusi

makovu ya chunusi

Chunusi ni tatizo la ngozi linalojitokeza sana hasa katika umri wa kubalehe. Chunusi ni tatizo kawaida la ngozi linalotokea kwenye sehemu za ngozi ambapo kuna tezi za jasho zinazojulikana kama sebaceous follicles. Kitendo cha kukwangua au kutusua inaacha makovu ya chunusi, kovu ambalo litakuharibia urembo wako wa asili.

Je nini kinasababisha chunusi?

Kama tulivoona pale juu, chunusi zinatokea sana nyakati za kubalehe na zinatokana hasa na mabadiliko ya vichocheo vya uzazi katika kipinddi hicho cha kupevuka. Mabadiliko haya yanatokea kwa wote mwanamke na mwanaume. Chunusi nyingi huwa zinaisha zenyewe kadiri mtu anavokua kiumri, ila muda wa kuisha natofautiana kwa kila mtu. Kukwangua sana chunusi kunafanya ubaki na makovu.

Hapa kuna baadhi ya tiba za nyumbani za kupunguza makovu ya chunusi na kurudisha urembo wako asili bila kutumia cream, losheni a mafuta yenye kemikali.

1.Juisi ya Limau kuondoa makovu ya chunusi

Limau lina asidi iitwayo ascorbic ambayo inaweza kusaidia kupunguza makovu. Paka juisi safi ya limau kwenye eneo lenye makovu na acha kwa dakika 10 kabla ya kuosha uso wako kwa maji safi. Epuka kufanya hivi kama una majeraha ya wazi au ngozi iliyojeruhiwa ama na kidonda.

2.Mafuta ya mzeituni ama olive

Mafuta ya mzaituni licha ya kusaidia wenye presha na magonjwa ya moyo, yanaleta matokeo mazuri sana kwenye kupunguza makovu ya chunusi. Paka mafuta kidogo ya olive kwenye ngozi iliyoharibiwa mara moja au mbili kwa siku baada ya kuoga. Hakikisha unanunua mafta original ya olive ili upate matokeo haraka.

3.Asali

Asali ina viambata vya uponyaji,na pia ni nzuri kwa afya ya ngozi. Paka asali kwenye eneo lenye makovu na acha kwa muda kabla ya kusafisha uso wako. Unaweza pia kuchanganya asali na juisi ya limau kwa matokeo bora. zaidi.

4.Aloe Vera

aloe vera

Gel ya aloe vera ina uwezo wa kupunguza uvimbe na inaweza kusaidia kupunguza makovu. Paka gel safi ya aloe vera kwenye eneo lenye makovu na acha kwa muda wa nus saa kabla ya kuosha uso wako. Unaweza pia kutumia vidonge vya aloevera kumeza ili kupnguza mafuta mabaya kwenye mwili.

5.Mafuta ya Nazi kuondoa makovu ya chunusi

Mafuta ya nazi yanaweza kusaidia kupunguza makovu na kuboresha afya ya ngozi. Paka mafuta ya nazi kwenye eneo lenye makovu na masaji kidogo kwa dakika chache kabla ya kuosha uso wako. Tumia mfululizo kwa mwezi mmoja ili kuona matokeo mazuri.

6.Mafuta ya Tea Tree

Mafuta ya tea tree yana uwezo wa kuua vimelea wa bakteria. Matmizi yake kwenye kuondoa makovu, changanya tone moja au mawili ya mafuta ya tea tree na maji na tumia kwa eneo lenye makovu kwa kutumia pamba. Epuka kusugua sana.

7.Tangawizi

Tangawizi ina uwezo mkubwa wa kupunguza uvimbe na kuboresha ngozi. Ponda tangawizi na changanya na maji ili kufanya mchanganyiko laini. Tumia kwenye eneo lenye makovu na acha kwa dakika 15 kabla ya kuosha uso wako.

8.Punguza Uvutaji Sigara

Kuvuta sigara kunaweza kusababisha kuchelewesha uponyaji wa makovu. Kujiepusha na uvutaji sigara kunaweza kusaidia ngozi kupona haraka. Jiwekee malengo leo ya kuacha sigara siyo tu kwa ajili ya ngozi, bali utaepuka na magonjwa mengine kama saratani ya mapafu.

9.Kula Vyakula Vyenye Lishe

Kula vyakula vyenye afya kama matunda, mboga mboga, protini za kutosha na virutubisho muhimu kunaweza kuboresha afya ya ngozi na kusaidia uponyaji wa makovu.

10.Ute mweupe wa yai kuondoa makovu ya chunusi

Matumizi ya ute mweupe wa mayai kama mask ya uso yanaweza kuwa na manufaa makubwa katika kuondoa makovu ya chunusi. Matumizi ya muda mrefu, hata usiku kucha yanashauriwa ikiwa unaweza kuvumilia harufu. Baadaye, inaweza kusafishwa na maji baridi. Hii inafanya kazi kimaajabu sana katika uponyaji wa makovu ya chunusi na kupunguza uvimbe wa ngozi.

Kama unajisikia vizuri, unaweza kuchanganya matone machache ya juisi ya limau na ute mweupe wa mayai na kisha kuutumia. Njia hii ya kuondoa makovu ya chunusi ni kwa wale ambao hawana aleji au mzio wa mayai.

Kumbuka, tiba za nyumbani zinaweza kutoa matokeo tofauti kwa kila mtu, na inaweza kuchukua muda kabla ya kuona mabadiliko. Ikiwa una wasiwasi kuhusu makovu ya chunusi au ikiwa hali inazidi kuwa mbaya, ni vyema kumwona daktari au dermatologist ili kupata ushauri na matibabu zaidi.

Angalizo

Endapo umeshaanza tiba ya hospitali usikatishe njiani. Lengo letu siyo kukufanya uache matibabu ya daktari wako. Lengo letu ni kukusaidia upate nafuu wakati unajiandaa kwenda hospitali. Kama njia zote hizi hazijakupa matokeo mazuri, tafadhali nenda hospital mapema muone daktari. Yawezekana kuna tatizo kubwa kiafya linalohitaji uangalizi wa karibu na vipimo zaidi.