Tiba ya nguvu za kiume bila dawa za kemikali

1.Kitunguu Saumu

kitunguu kutibu nguvu za kiume

Kitunguu saumu ni kitu cha kawaida kabisa kinachopatikana kila nyumba na sokoni pia. Kitunguu saumu ni tiba yako kubwa sana ikiwa unapungukiwa nguvu za kiume. Hii husaidia kuongeza mzunguko wa damu kwenye viungo vya uzazi. Pia ni kichocheo bora cha neva. Kitunguu saumu ina kiambata cha kemikali kinachoitwa allici, kimbata ambacho kinafahamika zaidi kuimarisha usafirishaji taarifa. Hasa huongeza mzunguko wa damu kwenye viungo vya uzazi wa kiume. Pia kitunguu saumu kinajulikana kwa uwezo mkubwa wa kupunguza mafuta mabaya kwenye damu.. Kwa hivyo, inaweza kusaidia kutibu tatizo la ugumu wa uume linalotokana na kiwango kikubwa cha mafuta ya kolesteroli katika damu.

2.Karafuu

karafuu

Hii pia ni mimea ya kawaida katika jikoni ya kila mtu, lakini yawezekana kabisa hujui kama ndio tiba yako rahisi na ya uhakika kwa nguvu za kiume. Karafuu ina uwezo mzuri sana wa kuamsha hisia na misuli ya uume, ambayo ni muhimu sana kwa wanaume wenye tatizo hili. Kula karafuu 2 kila siku baada ya chakula itakuwa na manufaa zaidi katika hali hii. Pia unaweza kunywa chai ya karafuu yenye mchanganyiko wa limau na asali kila siku asbhi na jioni.

3.Kitunguu Maji kutibu nguvu za kiume

Kitunguu maji ni kiungo kikuu katika karibu mapishi yote nyumbani. Lakini leo nataka nikwambie kwamba kitunguu ni tiba nzuri ya nguvu za kiume kama ulikuwa hujui. Kitinguu kina uwezo mkubwa wa kuchochea hisia na mwamko kwenye misuli ya uume na kuongeza mzunguko wa damu. Husaidia kuongeza idadi ya manii kwa mtu binafsi. Ubora wa manii huongezeka kwa kula vitunguu safi kawaida. Tafuta kitunguu kimoja kila siku, unaweza kukata na kuchanganya na nyanya na kaorti na kutumia salad.