Pumu ni ugonjwa ambao unashambulia watu wa pande zote za dunia, na inakadiriwa kuwa karibu watu milioni 300 wana ugonjwa huu duniani. Ni ugonjwa ambao hushambulia watu wa jinsia zote na rika zote lakini mara nyingi zaidi watu hupata ugonjwa huu utotoni. Watoto wengi huanza kupata dalili za ugonjwa huu wanapofikia umri wa miaka mitano. Watoto walio kwenye hatari kubwa zaidi ya kupatwa na maradhi haya ni wale wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo, wale wanaolelewa kwenye mazingira yenye moshi wa sigara na wale wanaozalia kwenye familia zenye kipato kidogo.
Watoto wenye ngozi nyeusi wanakuwa hatarini zaidi kuliko weupe. Mambo mengine yanayochangia ni mtoto kuwa na mzio (allergy) wa kitu fulani na/au kuzaliwa na wazazi wenye asili ya kuwa na maradhi haya. Watoto wa kiume hupata ugonjwa huu zaidi ya watoto wa kike lakini hali hubadilika wanapokuwa wakubwa. Katika ukurasa huu tutaona ni nini tiba ya pumu na jinsi ya kufanya ukiwa na ugonjwa huu ili uweze kuishi na kufanya shughuli zako za maisha bila kusumbuliwa na maradhi haya.
Aina za Pumu
- Pumu ya utotoni (child onset asthma)-aina hii ya pumu inatokea baada ya mtoto kuwa kwenye vizio kama vile vumbi la wadudu kama memnde, manyoya ya wanyamakam paka, mbwa na pia kutumia wipes zenye harufu kali (perfume) pumu hii hutokea kwa kuwa mwili wa mtoto hutengeneza kinga ya mwili (antibodies) zinazosababisha pumu.
Ugonjwa wa pumu ni sugu sana kwa watoto wanaozaliwa na uzito mdogo wenye asili ya kiafrika pia pumu ya utotoni huwaathiri zaidi watoto wa kiume. - Pumu ya ukubwani (adullt onset Asthma)-Pumu hii huanza baada ya kufika miaka 20, pumu hii huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume na pia haitokei sana kama pumu ya utotoni, vizio kama vile perfume, cream zenye harufu kali,sabuni nk ndio husababisha pumu hii kwa asilmia kubwa.
- Pumu itokanayo na mazoezi (exercise induced Asthma)-Pumu hii huwatokea zaidi wanaofanya mazoezi, ikiwa utakohoa na kukosa pumzi wakati wa mazoezi au baada ya mazoezi kuna uwezekano wa wewe kuwa na pumu ambayo inasababishwa na mazoezi pia hata kama sio mwana mazoezi kukimbia kwa kasi angalau dk 10 kunaweza kusababisha kukosa pumzi kwa muda mrefu na kuonyesha kwamba una pumu.
- Pumu itonakanyo na kukohoa sana(Cough induced Asthma); hii ni aina ya pumu ambayo ni ngumu sana na huumiza vichwa vya madaktari kuigundua kwasababu katika pumu hii inawezekana isitokee hata dalili zingine zaidi ya kukohoa kitu ambacho madaktari wanalazimka kuchunguza sababu nyingine za kukohoa sana na kuhakiksha sio zinasababishwa na kukohoa huko.
- Pumu ya usiku (nocturnal asthma): pumu hii hutokea kati ya saa sita usiku na saa mbili asubuhi, pumu hii huamshwa na vumbi la wadudu rangi ya nyumba, na harufu ya gesi pia Mara nyingi wagonjwa wa pumu hii hushtuka usingizini wakati wa usiku wa manane baada ya kukosa pumzi
- Pumu ya ngozi (eczema)neno eczema ambalo ni neno la kigiriki na linamaanisha kututumka kwa sehemu ya nje ya ngozi hali ambayo huonekana pale mtu anapopata maradhi haya. Ugonjwa huu ni wa muda mrefu nikimaanisha kwamba mtu huweza kukaa na ugonjwa huu kwa muda mrefu ingawa si muda wote mwili huonyesha dalil za ugonjwa.
Matibabu na jinsi ya kujikinga na Ugonjwa wa pumu
Matibabu ya ugonjwa kwa hospital yapo ya aina mbili moja ni Ile ya dharura ili kutoa tu msaada, dawa hii ni zile zinazosaidia kutanua njia ya hewa ambazo zimesinyaa (Bronchopdilators) pia husaidia kulainisha misuli ya njia za hewa iliyosinyaa, aina ya pili ya matibabu ni kutumia dawa za steroid za kuvuta (inhaled corticosteroids)
Matibabu haya huwa chanzo cha matatizo mengine kutokana na kwamba dawa hizo ni za kemikali hivyo huwa si nzuri kwani hazimalizi tatizo zinampa mtu unafuu tu, pamoja na hayo ugonjwa huu unaweza kuzuilika kwa kuepuka kutumia vitu vyenye harufu kali kama pafyumu,sabauni zenye harufu kali, kuacha kuvuta bangi, sigara na kukaa mbali na harufu ya rangi
Tiba asili kupitia Mafuta ya Peppermint na Eucalyptus
Mafuta haya yamekuwa yakitumika kwa zaidi ya miaka 2000 kutibu changamoto za mfumo wa hewa. Uzuri wa mafuta haya ni bei nafuu lakini ni ya asili yasiyo na kemikali. Hakikisha tu unapata kutoka kwa msambazaji wa kuaminika.
Huhitaji tena kuagiza nje ya nchi tumefanya utafiti na kukuletea mafuta haya yasiyochakachuliwa ili upate matokeo mapema. Mafuta yetu yatakusaidia
- Kupunguza makali ya brochitis sugu, pumu na mzio
- Kuua vimelea wabaya kwenye mfumo wa hewa
- Kupunguza msongo wa mawazo na kuimarisha usingizi