Categories
Afya ya Akili

Msongo wa Mawazo

mawazo

Moja ya sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa afya na kusababisha vifo vingi ni msongo wa mawazo .

Athari za Msongo wa Mawazo

 • Msongo wa mawazo unasababisha uzito mkubwa na kitambi: Kuongezeka ovyo kwa uzito,kitambi na nyama uzembe ni tatizo linalohusiana na ,msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo unabadili jinsi mafuta yanavohifadhiwa ndani ya mwili kwa sababu ya kubadilika kwa vichocheo na kemikali mbalimbali zinavyozalishwa na mwili pale ambapo unakuwa na stress. Kwa mfano tafiti zinasema kuwa stress kupitiliza husababisha uzalishaji wa protini inayoitwa betatrophin ambayo ni kizuizi kwa vimeng’enya mafuta yaliyohifadhiwa kwenye mwili.
 • Msongo wa mawazo unasababisha kuvurugika kwa homoni za kike: Ovary ni mfuko wa mayai ya kike, yaani mahali ambapo mayai ya kike huzalishwa.Polycstic ovary syndrome au PCOS kwa kifupi ni ugonjwa unaosababishwa na kuvurugika kwa vichocheo vya kike unaowapata zaidi wanawake walioko katika kipindi cha kuzaa. Wanawake wenye PCOS huwa na ovary zilizotanuka na zenye vimbe za majimaji ndani yake. Hedhi isiyokatika au isiyo na mpangilio maalumu, uotaji wa vinyweleo vingi kupita kiasi, kitambi na nyama uzembe, hizi ni dalili ambazo zinaweza kutokea kwa mwanamke mwenye PCOS. Msongo wa mawazo husababisha mwili kutoa vichocheo kama androstenedione ambacho ni kisababishi cha awali cha tatizo cha kujaa majimaji mifuko ya mayai kwa wanawake.
 • Kupungua kwa uwezo wa Kufanya tendo la ndoa kwa wanawake na wanaume
 • Kuongezeka kwa shinikizo la damu na pia kupanda kwa sukari kwenye damu.

Njia mbaya za Kuondoa Msongo wa Mawazo

 • Kuvuta sigara
 • Kunywa pombe sana
 • Kula sana au kula kidogo
 • Kukaa kwenye TV au kompyuta, saa nyingi sana
 • Kujitenga na marafiki, familia na shughuli
 • Kutumia vidonge
 • Kulala sana
 • Kuahirisha mambo
 • Kufanya kazi kupita kiasi ili kukimbia matatizo

Njia Salama za Kukabiliana na Msongo wa Mawazo

 1. Kukwepa Vyanzo Vya Msongo wa Mawazo: Siyo rahisi kukwepa kila chanzo cha msongo wa mawazo na ni vibaya kukwepa chanzo cha msongo wa mawazo ambacho inabidi ukikabili. Tumia njia hizi kukwepa chanzo cha msongo wa mawazo
  • Jifunze kusema hapana: Tambua uwezo wako wa kimwili na kikazi na zingatia kufanya kazi kulingana na uwezo ulio nao. Kuchukua majukumu zaidi ya uwezo ni chanzo cha kujipa msongo wa mawazo.
  • Wakwepe watu wanaokusababishia msongo: Kama kuna mtu anakusababishia msongo wa mawazo kila wakati, punguza muda wa kukutana naye au vunja kabisa mahusiano naye.
  • Dhibiti mazingira mabovu: Kama habari za jioni za kwenye TV zinakukera, zima TV na kama msongamano wa magari kwako ni kero chukua njia nyingine isiyo na msongamano hata kama ni ndefu zaidi.
  • Kwepa mada zinazokupa maudhi: Kama mada za dini au siasa hukupa maudhi, acha kushiriki kwenye mada hizo. Kama kila siku unalumbana na watu fulani kuhusu mada fulani, acha kuanzisha mada hizo au tafuta kisingizio cha kuondoka mada hizo zinapoanzishwa.
  • Chunguza ratiba yako: Itazame kwa kina ratiba yako, majukumu yako na kazi ulizojipangia kwa siku. Kama mambo ni mengi mno, yagawanye kwenye makundi ya yale ambayo ni lazima yafanywe na yale ambayo ni muhimu kufanyika. Yale ambayo si ya lazima sana yaweke chini kabisa kwenye ratiba au yaondoe kabisa.
 1. Badili Mazingira ya chanzo:
  Kama inashindikana kukwepa chanzo cha msongo wa mawazo, badilisha mazingira yake. Jaribu kufikiria ni nini cha kufanya ili chanzo hicho kisijitokeze tena hapo baadaye, hii inamaanisha kubadili namna yako ya mawasiliano au namna unavyoendesha shughuli zako.
  • Onyesha hisia zako: Kama kuna kitu au mtu anakukera, mweleze wazi kabisa kwa njia ya kistaarabu. Kama husemi, unajenga chuki na kuiacha hali ikibaki pale pale.
  • Tumia muda wako vizuri: Kushindwa kutumia muda wako vizuri ni chanzo kikubwa cha kupata msongo wa mawazo. Unapokuwa umechelewa kukamilisha jambo lako, utalifanya bila utulivu na utakosa umakini. Lakini ukiwa na mpango mzuri wa muda wako, utafanya kila kitu mbele yako kiufanisi na bila kupatwa na msongo wa mawazo.
 1. Badilika Kuendana Na Chanzo:
  Kama huwezi kukibadili chanzo cha msongo wa mawazo, wewe badili mtazamo wako kuhusu chanzo hicho:
  • Kitazame chanzo kwa mazuri yake: Kitazame chanzo cha kero kwako kwa kutazama mazuri ambayo yanaweza kupatikana kutokana na chanzo hicho. Badala ya kulalamika na kukasirika kutokana na foleni ya magari, chukulia kuwa huo ndio muda mwafaka kwako kujipumzika au kusikiliza muziki unaaoupenda ndani ya gari yako.
  • Kuwa na mtazamo wa jumla: Litazame jambo linalokukera kisha jiulize kama ni jambo litakalokusumbua kwa muda gani, mwezi mmoja, mwaka na jee mwisho wa siku ni madhara gani yatakayotokea. Kama ni suala la mpito tu, elekeza nguvu zako kwenye mambo mengine.
  • Rekebisha viwango vyako: Moja ya sababu ya kujipa msongo wa mawazo ni kutaka kila kitu kiende sawa kwa kiwango cha hali ya juu. Usijiweke kwenye mtego wa kushindwa kwa kujiwekea viwango vya juu kiufanisi. Jiwekee viwango vinavyowezekana kwako na kwa wenzako na jifunze kukubali matokeo ambayo hayakufika kiwango lakini siyo mabaya.
 1. Kubaliana Na Yale Ambayo Huwezi Kuyakabili:
  Vyanzo vingine vya msongo wa mawazo huwezi kuvibadili wala kuvizuia. Huwezi kukizuia kifo cha mtu wa karibu yako, wala ugonjwa mkubwa, au mporomoko wa uchumi wa nchi. Hapa inafaa kukubaliana na hali ingawa ni vigumu, lakini ni bora kuchukua msimamo huo kuliko kugombana na kitu usichoweza kukibadili.
 2. Pumzisha Na Burudisha Mwili Wako
  Mwili wako utapata uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na msongo wa mawazo endapo utaulea kwa kupata muda wa kuupumzisha na kuuburudisha kwa ufanya yafuatayo:
  • Fanya matembezi
  • Pumzika kwenye bustani au sehemu zenye mazingira ya asili
  • Mkaribishe rafiki nyumbani
  • Pata kikombe cha chai au kahawa
  • Jishughulishe kwenye bustani
  • Soma kitabu kizuri
  • Sikiliza muziki
  • Angalia vichekesho
  • Cheza na mnyama uliyemfuga

Tiba kupitia Mafuta Asili ya Lavender

lavender oil
mafuta ya lavender

Kwa miaka ya hivi karibuni mafuta ya lavender yamekuwa ni kitu adimu na cha kuaminika zaidi kutokana na uwezo wake kukukinga dhidi ya matatizo ya neva. Usimeze tena vidonge ambavyo vitakupa madhara makubwa kwa siku za mbele ikiwemo kupanda presha na stroke.

Matumizi: ili kupunguza msongo wa mawazo na athari zake: Chovya kiasi kidogo cha mafuta kwenye kidole kisha pakaa mafuta haya kwenye paji la uso, nyuma ya shingo na nyuma ya masikio kila unapotaka kwenda kulala, tumia mfululizo kwa mwezi mzima.

Kutokana na uhitaji wake mkubwa mafuta fake ya lavender yemekuwa mengi mtaani, hakikisha unapata mafuta original ili ufurahie faida zake.

Kwa upande wetu tumeamua kufanya utafiti na kukuletea mafuta salama yasiyochakachuliwa. Huna tena haja ya kuagiza nje ya nchi. Fika ofisini kwetu ama ukiwa mkoani tupigie ili tukutumie mafuta haya adimu.

Gharama ya mafuta ni Tsh 20,000/=
Tunapatikana Mwembechai Magomeni, Tupigie kwa namba 0762336530 au

Leave a Reply