Kukojoa kitandani

Kukojoa kitandani ni moja kati ya matatizo ya kawaida yanayojitokeza kwa watoto wadogo, ambapo mtoto hukojoa kitandani bila kujitambua. Watoto hawa wanakojoa zaidi wakati wa usingizi, hasa usiku, wakati muda wa kulala ni mrefu. Sababu kuu inaweza kuwa size ndogo ya kibofu cha mkojo. Sababu nyingine inaweza kuwa ni woga fulani au tatizo la kurithi.

Kama mzazi tambua haupo peke yako

Wazazi huchukua kila jitihada kumaliza tatizo hili haraka iwezekanavyo ili kuficha aibu. Kama mzazi nayempambania mtoto wako, tambua tu kwamba kuna njia asili nyingi ambazo zinaweza kumsaidia mtoto kuepuka kukojoa kitandani.

unahitajika uvumilivu na kutokata tamaa

Unatakiwa tu utambue kwamba tabia ya mtoto kukojoa kitandani haitatoweka ndani ya siku chache baada ya kutumia tiba za nyumbani, bali itahitaji nidhamu na uvumilivu zaidi. Hivyo basi, wazazi wanahitaji kuwa na subira zaidi na kufuata tiba hizi kwa kipindi kirefu cha miezi miwili ili kushuhudia mabadiliko.

Aidha, watoto wanapaswa kufundishwa kuhusu tabia za kwenda chooni na kuhakikisha haendi kulala bila kwenda chooni.

Hatua 7 za kutibu kukojoa kitandani

1.Mdalasini

madalasini ni tiba ya kukojoa kitandani

Ukiwa kama mzazi mwelekeze mtoto matumizi ya mdalasini wa unga kila siku ili kulishinda tatizo la kukojoa kitandani usiku. Mdalasini unajulikana kuwa ni tiba rahisi inayosaidia kudumisha joto la mwili, hivyo kuzuia kukojoa wakati wa kulala. Kwa njia nyingine, asubuhi kila siku, unaweza kutengeneza chai, na kweka nusu kujiko cha mdalasini na kumpa mtoto.

2.Mustard powder(haradali)

Nusu kijiko cha chai cha unga wa mbegu za haradali ukichanganywa na kikombe kimoja cha maziwa ya uvuguvugu kidogo kinapaswa kutolewa kwa mtoto, saa moja kabla ya kulala. Mbegu za haradali ni nzuri sana katika kutibu matatizo yote ya mkojo. Fanya hivo kila siku kwa miezi miwili, uone matokeo mazuri.

3.Asali ni tiba ya kukojoa kitandani

Asali, chanzo kizuri cha sukari asili, ni muhimu sana katika kutibu tatizo la kukojoa kitandani. Kijiko kimoja cha asali kabla ya kwenda kulala kinaweza kusitisha kabisa tatizo la kukojoa kitandani kwa watoto. Asali inaweza kutolewa ikichanganywa na maziwa, wakati wa kifungua kinywa cha asubuhi au watoto wanaweza kula moja kwa moja kwa kulamba kijiko kimoja asbhi kabla ya kula na jioni kabla ya kulala.

4.Mazoezi ya kibofu

Mfundishe mtoto wako mazoezi ya kibofu ambayo yatasaidia kudhibiti kibofu na kuimarisha misuli ya kibofu. Mpe mtoto kiasi kikubwa cha maji kipindi chote cha mchana na umpeleke afanye zoezi la kubana mkojo kwa muda fulani.

pale anapordia zoezi, mtoto atajifunza kudhibiti kibofu na hii itakuwa na manufaa katika kudhibiti misuli ya kibofu usiku pia. Hii ni muhimu kwa watoto waliozidi umri wa miaka mitano, ambao wanaweza kufanya mazoezi haya kwa urahisi zaidi.

5.Punguza Vinywaji Usiku

Hakikisha mtoto anakunywa zaidi wakati wa mchana na kidogo wakati wa jioni na kidogo kabisa wakati wa usiku. Karibu asilimia 40 ya maji yanapaswa kunywewa kati ya saa 1 asubuhi hadi saa 6 mchana, asilimia nyingine 40 kati ya saa 6 mchana mpaka 12 jioni. Na kisha asilimia 20 tu baada ya saa 12 jioni.

Hata hivyo, watoto wanaoshiriki katika michezo au shughuli za kimwili au michezo jioni, hawapaswi kuzuiliwa kunywa maji hata baada ya saa 5 mchana. Aidha, kama watoto wanapendelea kunywa zaidi wakati wa jioni, usizuie, kwani maji ni muhimu sana kwa afya na kuzuia ukosefu wa maji mwilini.

6.Kukojoa Mara Mbili Kabla ya Kulala

Mhamasishe mtoto kuondoa mkojo kabisa kwa kwenda chooni mara mbili, mara moja wakati wa mchakato wa kulala, na mara nyingine, muda mfupi kabla ya kulala kabisa. Mhamasishe kutumia choo pia wakati wa usiku, ikiwa inahitajika. Msaidie mtoto kwenda chooni usiku mpaka aweze kufanya mwenyewe.

7.Kukosa choo inachangia kukojoa kitandani

Kwa watoto, mara nyingine kama ana shida ya kukosa choo mda mrefu, kunaweza kuwa sababu ya kukojoa kitandani usiku. Hakikisha mtoto anapata choo mara kwa mara kwa kumpa vyakula asili, matunda na mboga za majani. Kama utashindwa kumtibia nyumbani basi usisite kumuona daktari ili apate dawa ya kusafisha kinyesi.

Angalizo

Endapo umeshaanza tiba ya hospitali usikatishe njiani. Lengo letu siyo kukufanya uache matibabu ya daktari wako. Lengo letu ni kukusaidia upate nafuu wakati unajiandaa kwenda hospitali. Kama njia zote hizi hazijakupa matokeo mazuri, tafadhali nenda hospital mapema muone daktari. Yawezekana kuna tatizo kubwa kiafya linalohitaji uangalizi wa karibu na vipimo zaidi.