Historia inasema kwamba mafuta ya olibanum yalianza kutumika muda mrefu huko mashariki ya kati na uarabuni, kwa wakristo wanaamni kwamba mamajusi watatu walipoenda kumuona mzaliwa Yesu walipeleka pia mafuta haya ya olibanum au kwa jina lingine frankincense.
Inaaminika pia enzi za utawala wa dola ya Kirumi mafuta haya yalitumika kama mafuta matakatifu wakati wa sherehe za kidini na kwenye kutoa sadaka.
Mafuta ya olibanum au kwa jina lingine frankincense hupatikana baada ya kuchakatwa kwa utomvu wa mimea ya Boswellia sacra na Boswellia carteri. Mimea hii inapatikana zaidi Africa ya Magharibi nchi za Somalia na Ethiopia , na uarabuni nchi za Yemen na Oman, huku nchi ya Oman ikiwa ndo mzalishaji mkuu wa mafuta haya.
Faida za Mafuta ya olibanum/frankincense
Mafuta haya yanaaminika kusaidia kwa changamoto za kiafya kama
- Magonjwa ya viungo kama arthritis au rheumatoid arthritis
- Mafua na mfumo wa upumuaji:mafuta yanasaidia kusafisha njia ya hewa na hivo kuimarisha upumuaji wa wagonjwa wa asthma, mafua makali na kuziba kwa njia za hewa.
- Afya ya kinywa: magonjwa ya kinywa kama harufu mbaya, meno kuuma, kuvimba kwa fizi na kuvimba kwa mdomo yanaweza kutibika kupitia mafuta ya olibanum
- Kwenye uzazi; mafuta haya husaidia kurekebisha homoni kwa wanawake na pia kurekebisha mzunguko uliovurugika, kupunguza hatari ya kupata saratani ya kizazi.
- Kwa wagonjwa wa goiter: mafuta ya olibanum yanasaidia kupunguza mpambano (inflammation) kwenye tezi ya thayroid na hivo kusaidia kupunguza kwa uvimbe shingoni .
Jinsi ya Kutumia mafuta ya olibanum/frankincense
Ili kufurahia faida za mafuta haya pakaa mafuta kwenye ngozi ya mwili. Hakikisha tu unachanganya mafuta ya olibanum na mafuta mengine kama jojoba, nazi, olive au mafuta ya almond.
Unaweza pia kuweka kwenye diffuser yako ama ukachanya na maji ya kuoga ukafurahisa faida zake.
Je mafuta ya Olibanum ni Salama kutumika muda wote?
Kiujumla mafuta ya olibanum ni salama kabisa, isipokuwa kwa makundi machache tu ndipo hayaruhusiwi kutumia mfano wajawazito na wanaonyonyesha, kwa mjamzito inaweza kusababisha mimba kuharibika.