Tiba aina 4 za uhakika kuondoa Makovu ya uzee

makovu ya uzee

Makovu ya uzee mara nyingi hujulikana kama liver spots au sun spots na huwa ni doa jekundu au hudhurungi kwenye ngozi, ambazo kwa kawaida hutokea kwenye uso, mikono, na shingo. Katika kesi nyingi, madoa haaya huwa yanaongezeka kutokana na miale ya jua.

Pia madoa ya uzee yanaweza kutokea wakati ini linakuwa limezidiwa na sumu. Kwa bahati nzuri, dalili za kwanza za makovu haya ya uzee yanaweza kutibiwa na kutatuliwa kwa urahisi kwa msaada wa tiba rahisi za nyumbani bila hata. Hebu tuzame sasa katika baadhi ya tiba muhimu za nyumbani za kupunguza makovu ya uzee.

Tiba za Nyumbani kwa Makovu ya Uzee

1.Siki ya Tufaha (Apple Cider Vinegar)

vinegar kuondoa makovu ya uzee

Pale ukichukua mchanganyiko wa siki ya tufaa na juisi kitunguu maji kisha ukapakaa kwenye makovu yako utaona maajabu sana. Asidi ya kitunguu saumu na tufaha husaidia kuyafifisha haya makovu na kukuacha ukiwa na urembo kama kijana mdogo.

Hakikisha umechanganya kizibo kimoja cha siki ya tufaa na maji vijiko vitatu kabla ya kutumia. Unaweza pia kuchanganya siri ya tufaha na maji ya uvuguvugu na kunywa mchanganyiko huu mara moja kila siku, nusu saa kabla ya kula li kupata ngozi laini na bila makovu ya uzee.

2.Juisi ya Aloe Vera

Juisi ya aloe vera pia inasemekana kuwa yenye ufanisi katika matibabu ya makovu ya uzee. Wengi wameona matokeo mazuri na ndio maana ninakwelekeza na wewe bure kabisa ili uondoe uzee kwenye ngozi yako. Matumizi: Paka kiwango kidogo cha jisi au maji ya aloe vera moja kwa moja kwenye makovu ya uzee kisha fanya masaji kwa dakika 5, subiri nusu saa kisha osha uso kwa maji ya uvuguvugu. Utaanza kuona mabadiliko ya kiasi kikubwa na kuonekana mrembo/mtanashati ndani ya mwezi mmoja.

3.Juisi ya Ndimu kuondoa makovu ya uzee

Tiba nyingine nzuri ya nyumbani ni kutumia juisi ya ndimu kupunguza makovu ya uzee, madoa, na kasoro za ngozi. Chukua juisi ya ndimu na upake moja kwa moja kwenye makovu ya uzee. Ikiwa juisi ni kali sana, unaweza kuichanganya na maziwa ya mtindi na kisha kuipaka kwenye uso. Mtindi utaacha ngozi yako laini na juisi ya ndimu itasaidia kufifisha makovu ya uzee. Fanya zoezi hili kila siku kwa week mbili mpaka mwezi kupata matokeo mazuri.

4.Mafuta ya Mbono (Castor Oil)

mafuta ya mbono

Inaaminika kuwa mafuta ya mbono ni tiba muhimu ya nyumbani ya kupunguza makovu ya uzee. Paka mafuta ya mbono kwenye makovu ya uzee kwenye uso na shingo kila siku asbuhi na jioni baada ya kuoga ili upate matokeo mazuri.

Angalizo

Endapo umeshaanza tiba ya hospitali usikatishe njiani. Lengo letu siyo kukufanya uache matibabu ya daktari wako. Lengo letu ni kukusaidia upate nafuu wakati unajiandaa kwenda hospitali. Kama njia zote hizi hazijakupa matokeo mazuri, tafadhali nenda hospital mapema muone daktari. Yawezekana kuna tatizo kubwa kiafya linalohitaji uangalizi wa karibu na vipimo zaidi.