Tiba za Nyumbani kwa Mashimo ya Meno na meno kuoza
Kusafisha uchafu sugu na ktibu mashimo ya meno yaliyosababishwa na meno kuoza si kazi rahisi. Yahitaji utayari, kutenga muda, na huduma ya kutosha kwa jino au meno yaliyoathiriwa ili kudhibiti shimo na kurejesha ukuaji wa bakteria kwenye meno yaliyoathiriwa.
Kuna vitu vingi sana vya asili ambavyo vinapatikana nyumbani kwako, ambavyo ni tiba nzuri sana. Ni vile tu hujapata mtaalamu wa kkwelekeza nini cha kufanya. Na leo kupitia ukurasa huu nitakpa siri za kutibu meno yako bila kuyang’oa.
1.Kusukutua na Chumvi
Changanya kiasi cha kutosha cha chumvi katika maji ya uvuguvugu kisha sukutua na suluhisho litapatikana. Unaweza kufanya hivi kati ya mara nne hadi kumi kwa siku na hata zaidi ikiwa maumivu ni makali sana au maambukizo yameenea sana.
Maji ya chumvi husaidia kuua bakteria kwenye mdomo, meno, na koo kwa kufanya kama wakala hodari wa kupambana na bakteria katika eneo zima. Pia chunvi inasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa nafasi za kuongezeka kwa maambukizi ya bakteria kwenye jioni lingine.
2.Mafuta ya Mdalasini
Mafuta ya mdalasini ni kiungo chenye nguvu ya kuua bakteria wabaya kwenye jino lako na hivo kuzuia jino kuoza na kutoboka.Weka matone machache ya mafuta kwenye shimo la jino kwa kutumia pamba usiku kabla ya kulala, itasaidia kupunguza maumivu ya shimo la jino.
Mafuta ya mdalasini yamejulikana kwa muda mrefu kuwa na uwezo mkubwa wa ktibu magonjwa ya meno. kama umekosa mafuta unaweza tu kuweka unga wa karafuu kwenye jino lililoathiriwa. Ikiwa unatumia mafuta, uwe mwangalifu wakati wa kutumia, kwani yanaweza kuharibu tishu laini za mdomo, kusababisha uvimbe.
3.Maji ya Uvuguvugu
Endapo maji ya uvuguvugu yakitumiwa ipasavyo kwenye sehemu zilizoathiriwa za mdomo husaidia kupunguza ukuaji wa bakteria wabaya kwenye jino. Pia maji yanafanya iwe rahisi kwa mafuta ya meno na dawa za kusukutua kufanya kazi vizuri dhidi ya maambukizi. Kikawaida ni wazo zuri kusafisha mdomo wako na maji ya uvuguvugu kabla ya kwenda kulala na baada ya kuamka, na angalau mara moja kipindi cha mchana hasa kama umekula vitu vya sukari, ili kuondoa uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi.