Kuondoa Weusi Chini ya Macho Bila dawa wala upasuaji

Ngozi chini ya macho ni nyembamba na dhaifu zaidi kuliko sehemu nyingine za uso. Eneo hili la mwili halina tezi za jasho (sebacious gland) ambazo huwa zinazalisha mafuta asili kwenye ngozi. Ndiyo sababu ngozi chini ya macho si nyororo kama sehemu nyingine za ngozi na ni dhaifu zaidi. Ingawa ni kawaida kwa watu wazima, mara nyingine hata watoto pia huonekana wakiwa na mabaka na weusi chini ya macho.

Visababishi vya weusi chini ya macho

Mara nyingi chanzo inaweza kuwa ni kwa sababu ya maradhi, upungufu wa virutubishi. Pia inaweza kuwa kutokana na msongo wa mawazo na ukosefu wa usingizi. Sababu zingine zinaweza kuwa ni mzio, shinikizo la damu, au hata matumizi ya pombe. Wakati mwingine ujauzito au maambukizi ya pua yanaweza pia kusababisha weusi chini ya macho chini ya macho. Pia yanaweza kutokea kutokana na kuvuta macho kwa sababu ya vipele, kuwashwa, kuumwa, au tabia tu ya kuvuta macho kwa ndani mara kwa mara.
Tiba asili kuondoa weusi chini ya macho

1.Maji ya Barafu

Tumia kiwango kidogo cha maji ya barafu kila siku kwenye eneo lililoathiriwa. Chovya taulo safi ya uso kwenye maji baridi ya barafu, chuja maji yake, fumba macho yako na weka taulo hii kwenye macho yako. Badilisha taulo endapo ubaridi umeisha. Fanya tiba hii kwa dakika 15. Usiifanye kupita kiasi.

2.Maziwa ya Baridi

Maziwa ni kisafishaji asilia na hunawirisha ngozi yako. Paka maziwa ya baridi kwenye wesi wa macho na chini ya macho yako kila siku, safisha baada ya dakika 15. Hii itaondoa weusi kwenye macho na kurudisha urembo wako

3.Tango kuondoa weusi chini ya macho

Juisi ya tango ndiyo mbadala inayotumiwa zaidi na watu wengi kwenye urembo wa ngozi. Inapaswa kutumiwa mara mbili kwa siku kwa dakika 15 na kisha kusafishwa. Hakikisha unasaga tango na kupata juisi ili utumie vizuri. Unaweza pia kuchagua njia rahisi, weka vipande vyembamba vya tango kwenye macho yako na vikae kwa dakika 15.

4.Tango na limau

Juisi ya lima inaweza kuchanganywa na juisi ya tango na kutumiwa kwa dakika 15. Limau ni wakala mzuri wa kufanya ngozi kuwa nyeupe. Safisha na kwa dakika 15 na oshe ngozi yako kwa maji ya uvuguvugu.

5.Nyanya kuondoa weusi chini ya macho

Kila nyumba ina nyanya jikoni mwake, hii ni tiba muhimu na rahisi ya kuondoa weusi chini ya macho yako. Juisi ya nyanya inafanya rangi ya ngozi yako kuwa nyororo na nzuri. Tumia mchanganyiko huu walau kwa week 4 mfullizo ili uone matokeo mazuri zaidi.

6.Manjano

manjano

Kwa weusi chini ya macho, tumia manjano na juisi ya nanasi. Tengeneza mkorogo wenye majnajno na nanasi na itumie kwenye sehemu zilizoathirika. Acha kwa dakika 15 hadi 20 na suuza baadaye kwa maji ya uvuguvugu.

Lishe na Mtindo wa Maisha kwenye kutibu weusi kwenye macho.

  • Kunywa maji ya ktosha kila siku kuimarisha ngozi yako
  • Lala usingizi mnono kwa saa 6 hadi 8 kila siku.
  • kula matunda na mboga mboga kila siku, kila baada ya mlo wako
  • tumia miwani ya jua endapo utakaa nje mda mrefu maana miale inaharbu ngozi yako
  • Epuka Kuvuta Macho Epuka kuvuta macho yako kwa ndani