Mafuta ya Jasmine huzalishwa baada ya kuchakatwa kwa maua ya mimea ya Jasmine ambayo hukua na kufikia urefu wa futi 10 mpaka 15. Maua ya Jasmine hukua hasa nyakati za usiku . Kutoka uwezo wake mkubwa wa kutoa harufu nzuri, nchi kama Pakistan zimetambua maua haya na kuyapa hadhi ya kuwa maua ya taifa. Nchini India dini ya wahindu imetambua maua ya Jasmine kama maua matakatifu (holy flower).
Fida za Kutumia mafuta ya Jasmine
- Mafuta yanasifika kwa kuongeza hamasa kwenye tendo la ndoa. Itakusaidia kwa changamoto za kuwahi kufika kileleni na kushindwa kusimamisha uume. Mafuta haya yakitumika kuelekea kwenye tendo la ndoa yatakufanya ufurahie tendo na kuamsha hisia zako.
- Kurejesha ubora wa ngozi iliyoharibika; Mafuta haya yanafaa kwa ngozi iliyopauka, ngozi iliyoathiriwa na chunuia, magonjwa ya ngozi na kwa ngozi yenye aleji. Hata hivo usipakae mafuta haya kwenye kidonda au ngozi yenye jeraha maana italeta kuvimba na kututumka zaidi.
- Kupunguza maumivu wakati wa hedhi: Mafuta ya Jasmine yatakusaidia kupunguza maumivu kwa mwanamke anapokuwa kwenye siku zake na kurekebisha mzunguko uliovurugika.
- Kutuliza akili: Mafuta haya yaimarisha uwezo wa ubongo kufanya kazi na kukufanya mweye kujiamini na mwenye kufikiria chanya zaidi. Inaondoa hofu, msongo wa mawazo na hali ya kujiona mkosaji.
- Kutibu changamoto ya kukosa usingizi na sonona(depression)
Jinsi ya Kutumia mafuta ya Jasmine
Mafuta ya Jasmine yanaweza kutumika kwa namna mbalimbali kulingana na hitaji lako. Zifuatazo ni baadhi ya njia za kutumia na kufurahia tiba kwa mafuta haya.
- Tumia kifaa cha kupuliza (diffuser) – weka kiasi kidogo cha mafuta ya Jasmine kisha furahia hewa nzuri yenye harufu ya kusuuza.
- Kwa matumizi ya kwenye ngozi: pakaa kiasi kidogo cha mafuta ya jasmine kwenye shingo ama paji la uso ili kutumia akili na kufanya mwili wenye furaha na matumaini. Pakaa pia kwenye ngozi yako kama unahitaji kutibu magonjwa ya ngozi na maumivu ya misuli.
- Kuvuta hewa: ili kutbu kkohozi kikali na msongo wa mawazo chukua kiasi kidogo kwenye pamba ama kitambaa laini kisha vuta hewa yake mara nyingi.
Je Mafuta ya Jasmine ni Salama Kutumiwa na kila mtu?
Ni kweli mafuta haya ni salama kiujumla, hayana sumu kwa mwili. Hata hivo yatakiwa kutumiwa kwa uangalifu, matumizi makubwa yatakufanya kulegea na kushindwa kufanya kazi zako vizuri.Haitakiwi kumeza mafuta haya. Kama ni mjamzito ama unanyinyesha tunashauri usitumie mafuta ya Jasmine.
Kwa ajili ya kupaka kwenye ngozi inashauriwa kuchanganya mafuta ya jasmine na mafuta ya almond au mafuta na nazi.