Kipandauso ni maumivu makali ya kichwa yanayotokea hasa upande wa kushto juu ya jicho. Ni tatizo gumu linalohusisha ubongo na mishipa ya damu karibu na ubongo na kichwa. Kipandauso hutokea kutokana na mchanganyiko wa kututumka kwa mishipa ya damu na kutolewa kwa kemikali kutoka kwenye neva ambazo husababisha kuvimba, na maumivu. Kimsingi kipandauso, hutokea kutokana na mabadiliko ya kipenyo cha mishipa ya damu kichwani.
Nini hasa kinapelekea kipandauso?
Kwanza mishipa hukaza, kisha maumivu huanza na mishipa hufunguka. Pia hutokea kutokana na kutofautiana kwa homoni inayoratibu hisia yaani homoni ya serotonin. Homoni zina jukumu kubwa katika maendeleo ya kipandauso. Ndio maana wanawake hupata kipandauso zaidi kuliko wanaume na hasa kabla, wakati au baada ya hedhi. Hii ni kutokana na uhusiano kati ya homoni ya estrogen na kipandauso.
Visababishi vingine vya Kipandauso
Sababu kubwa ya kipandauso ni mabadiliko ya homoni. Wengi wa wanawake hupata maumivu ya kichwa wakati wa kipindi chao. Chakula ni sababu ya pili ya kawaida ya kipandauso. Pombe, tumbaku, chokoleti, kafeini, kiambatana cha monosodium glutamate (MSG) kinachopatikana zaidi kwenye vinjwaji, kukosa milo au kufunga, ini za kuku, divai nyekundu, nk.). Visababishi vingine ni mafadhaiko, msongo wa mawazo, njaa, na mabadiliko katika mazoea ya kulala, mabadiliko katika mzunguko wa hedhi, mzio, mwanga mkali, sauti kubwa, harufu na manukato fulani.
Tiba mbadala za kipandauso
1.Mafuta ya mnanaa yani Peppermint
Peppermint inajulikana kuwa inaleta utulivu na inaweza kufanya sehemu za mwili kupoa. Sifa hizi hufanya iwe na manufaa kwa watu wanaosumbuliwa na kipandauso. Paka mafuta ya pippermint kwenye paji la uso na nyuma ya sikio taratibu ili kupata nafuu kutokana na maumivu ya kichwa. Unaweza pia kuchua kwa ndani kama dawa. Wanawake wajawazito hawapaswi kutumia pippermint.
2.Mafuta ya mkaratusi
Mafuta ya mkaratusi huongeza usambazaji wa oksijeni kwenye damu na kuwezesha oksijeni na virutubisho zaidi kufikishwa kwenye seli. Mafuta ya mkaratusi hupunguza kuvimba na husaidia kusitisha kipandauso. Paka matone machache ya mafuta kwenye paji la uso, puani na nyuma ya masikio mara mbili kwa siku na hakikisha unamasaji dakika 3.
3.Kunywa Maji
Kipandauso cha wengi husababishwa na ukosefu wa maji mwilini. Kunywa maji mengi walau lita mbili kwa siku na ongeza iwango unafanya kazi ngumu ama unafanya mazoezi ama mcheza mpira. Maji yansaidia sana kupona kwa kipandauso.
4.Kitungu saumu
Kitunguu saumu kina uwezo wa asili za kupunguza kuvimba na kinaweza kusaidia kupunguza maumivu ya kichwa. Matumizi: menya punye 4 za kitunguu samu pondaponda kisha changanya na na mafuta ya mzeituni. Paka mchanganyiko huu kwenye paji lako la uso na paji la kichwa, kisha acha kwa dakika 30 kabla ya kuosha.
5.Mafuta ya Lavender kutibu kipandauso
Mafuta ya lavender yanajulikana sana kwa kutuliza maumivu na neva. Matumizi: Changanya matone machache ya mafuta ya lavender na mafuta ya nazi au mafuta ya mlozi, kisha paka kwenye paji lako la uso na shingo. Unaweza pia kuongeza matone machache ya mafuta ya lavender kwenye ndoo ya maji ya kuoga kisha oga yale maji taratibu usiku, kupumzisha mwili wako na kupunguza uchovu.