Giseng ni mmea unapatikana zaidi katika bara Asia ya kusini maeneo yenye baridi hasa kwa nchi za China, Korea na eneo la Siberia huko Urusi.
Mimea hii hupatikana pia Marekani. Mmea wa Ginseng uligunduliwa kwa mara ya kwanza na Wachina wa kale kwa zaidi ya miaka 5000 iliyopita, na umekuwa ukithaminiwa kwa kutibu magonjwa mengi ikiwemo saratani na kurekesha afya ya mwili kupitia vidonge na mafuta ya Ginseng
Kutokana na umbo la mmea huu kama binadamu, inaaminika kwamba unaweza kutibu magonjwa zaidi kama kisukari, presha, kuimarisha uwezo wa tendo la ndoa hasa kwa wanaume, kuondoa dalili mbaya kwa wanawake walikoma hedhi pamoja na kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mwili
Kazi na Faida za Mafuta ya Ginseng
- Kuimarisha misuli ya uume na uwezo wa tendo a ndoa: kampaundi zilizopo kwenye mafuta ya ginseng zinasaidia kuimarisha mzunguko wa damu wakati wa tendo la ndoa na hivo kukufanya uhimili tendo kwa muda mrefu pasipo kuchoka haraka.
- Kuimarisha kinga ya mwili na hivo kusaidia kupona mapema kwa wagonjwa wa saratani na TB.
- Kupambana na uchovu wa mwili na kurejesha guvu mwilini
- Kupunguza sukari kwenye damu: Mafuta ya ginseng ni mazuri kwa wagonjwa wa kisukari cha ukubwani(type 2 diabetes), japo ni muhimu yatumike kwa uangalifu kwani yanaweza kushusha sukari kupita kiasi.
Mafuta ya Ginseng yanawafaa watu wote kwenye makundi haya
- Wanaougua saratani za aina mbali mbali
- Waliopo kwenye tiba ya mionzi
- Walioathirika na ugonjwa wa ukimwili na kupungukiwa CD4
- Wanaopata uchovu mara kwa mara na mwili kukosa nguvu
Je kila mtu anaweza kutumia Mafuta ya Ginseng?
Mafuta ya ginseng yanatakiwa kutumika kwa uangalifu zaidi kwa wagonjwa wa sukari kwani yanaweza kushusha sukari zaidi. Wajawazito na wanaonyonyesha hawaruhusiwi kutumia mafuta haya ya ginseng. Kwa wagonjwa wanaotumia dawa za kuzuia damu kuganda zungumza na daktari kabla ya kutumia mafuta ya ginseng.