Mafuta ya mnanaa ama peppermint yanapatikana kupitia majani ya mmea wa mnanaa (Mentha piperita). Mmea huu hutumika hasa majumbani kama tiba asili ya matatizo ya tumbo, maumivu ya viungo na maumivu ya kichwa
Faida na Matumizi ya Mafuta ya mnanaa(peppermint)
- Kutibu na kuleta nafuu kwa magonjwa ya tumbo: Mnanaa una kiwango kikubwa cha kamapundi ya menthol ambacho kisaidia kuondoa mvurugiko wa tumbo na kukutibu changamoto za tumbo kujaa gesi, na maumivu eneo la juu la tumbo baada tu ya kumaliza kula.
- Kutuliza matatizo ya mfumo wa hewa- Mafuta ya peppermint yanakusaidia kufungua njia za hewa ili uweze kuvuta hewa safi na kupumua vizuri. Mafuta yanawafaa wagonjwa wote wa TB, wenye mafuta makali , kikohozi, wenye pumu.
- Kutuliza maumivu; Mafuta ya peppermint yanasaidia kutuliza maumivu ya misuli pale yanapotumika kwenye masaji. Unaweza pia kuchanganya mafuta haya na maji ya kuoga.
- Kupunguza kizunguzugu na kutapika kwa wagonjwa wa saratani walioko kwenye tiba ya mionzi.
- Kupunguza athari ya magonjwa ya virusi (HPV), kama unapata maambukizi ya mara kwa mara pakaa mafuta katika eneo lililoathirika na ufanye masaji.
- Kuimarisha ukuaji wa nywele: Ili kulinda nywele zako dhidi ya fangasi na bakteria, changanya kiasi kidogo cha mafuta ya mnanaa kwenye shampoo na mafuta ya nywele kabla ya kupakaa.
- Kuimarisha afya ya kinywa; Kama unanuka mdomo ama kuvimba fizi mara kwa mara, tumia mafuta ya mnanaa kuoshea mdomo
Je Mafuta ya Mnanaa/peppermint ni Salama kwa kila Mtu Kutumia?
Mafuta ya mnanaa ni salama yakitimia kwa kiasi kidogo lakini yanaweza kuleta madhara madogo madogo kwa watu wenye ngozi za kututumka(sensitivities), ni muhimu kwa mafuta haya kutumika kwa uangalifu kwa kufuata maelekezo ya mtaalamu wa tiba asili.
- Wanajawazito na wanaonyonyesha; mafuta yanaweza kusababisha maziwa kutoka mengi zaidi ama mimba kuharibika, kwahivo siyo salama kwa kundi hili kutumia mafuta ya mnanaa
2.Watoto chini ya miaka 7; wasitumie mafuta haya bila kuchanganywa na mafuta mengine - Weneye kisukari: kutumia mafuta ya mnanaa/peppermint yanaweza kupunguza sukari kupita kiasi, muhimu kufatilia sukari yako mara kwa mara.
- Wangonjwa wenye tatizo la acid-Gasroesophagual reflux disease na wanaitumia dawa za kupunguza acid wasitumie mafuta ya peppermint