Mafuta ya tangawizi yanapatikana kutoka kwenye mizizi ya mmea wa tangawizi kisayansi unaitwa (Zingiber officinale).
Tangawizi imejizolea sifa kubwa na kuanza kutumika tangu miaka ya zamani enzi za utawala wa Roma wakati huo tangawizi ikiuzwa zaidi kutoka uarabuni mapaka bara ulaya.
Inasemekana kwamba robo kilo ya tangawizi iliuzwa kwa mabadilishano ya kondoo mmoja.
Kwa miaka ya sasa tangawizi inaweza kutumika kwa namna mbalimbali. Unaweza kutafuna, ukasaga na kutengeneza chai au ukaweka kweye mboga. Tangawizi ikikauka unga wake unaweza kutumika kama tiba mbadala, ama yakatengenezwa mafuta ambayo atakutibu changamoto nyingi za kiafya.
Faida za Mafuta ya Tangawizi
Mafuta ya tangawizi yanasaidia kutibu changamoto zifuatazo za kiafya
- Magonjwa ya tumbo na shida ya choo: tangawizi inasaidia usagaji wa chakula na hivo inafaa kwa changamoto za kukosa choo na choo kigumu, tumbo kujaa gesi na kujamba sana, iakusaidia pia.
- Changamoto ya mfumo wa hewa; mafuta ya tangawizi yanaleta nafuu kwa tatizo la kikohozi, mafua makali na pia kusaidia kuzibua njia za hewa.
- Kupunguza maumivu ta mwili kwa kurekebsha homoni ya prostaglandins ambayo ndio huhusika na maumivu.
- Magonjwa ya moyo: kutumia mafuta ya tangawizi mara kwa mara yanapunguza hatari ya damu kuganda kwenye mishipa na kuziba kwa mishipa ya damu, kwasababu mafuta ya tangawizi yanapunguza mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol).
- Shinikizo la damu: tafiti zinasema kwamba watu wanaotumia tangawizi kila siku wanapunguza uwezekano wa kuugua presha ya kupanda kwa zaidi ya asilimia 8.
Je Mafuta ya Tangawizi ni Salama?
Mafuta ya tangawizi yakitumika kwa kiwango cha kawaida hayana shida kwasababu hayana kemikali zenye sumu.
Kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha watumie mafuta ya tangawizi kwa uangalifu. Ni vizuri pia kuongea na dakari wako kabla hujaanza kutumia mafuta ya tangawizi