Categories
Uncategorized

Mbinu 5 za kusimamisha matiti yaliyolala ukiwa nyumbani

kusimamisha matiti

Uzuri wa kike usio na mwisho ni mchanganyiko wa mambo kadhaa, na miongoni mwao ni matiti yaliyosimama vizuri, wanasema chuchu saa sita. Matiti yaliyolala yanaweza kuharibu sana uzuri wa mwanamke na hasa kupunguza mvuto wake kwa wanaume, na ndiomaana nataka leo nikufundishe njia asili za kusimamisha matiti yako.

Japo mwenzi wako anaweza asilalamike, lakini anavutiwa na picha ya matiti yaliyonyooka ya wanawake wengine. Ili kumvutia tena na kupata umbo lako la zamani ambalo lilimvutia mwenzi wako wakati anakutongoza, unahitaji kufanya tishu hizo zichangamke. Hii itasaidia kusimamisha matiti na kukupa tena ujasiri na mapenzi ya mwenzi wako.

Nini kinapelekea matiti kulala?

Kuna sababu kadhaa za kulegea kwa matiti yako kama vile kunyonyesha, lishe duni, magonjwa, kuvaa sidiria isiyofaa, kukoma hedhi nk. Siku hizi kuna njia kadhaa za kusimamisha matiti. Hata hivyo, njia inayotumiwa mara kwa mara ni upasuaji wa matiti. Lakini hii ni ghali sana, zaidi ya hayo, kuna athari zisizofurahisha za upasuaji wa matiti. Yanini sasa upate madhara wakati kuna njia za asili unazoweza kuzitumia nyumbani kwako kusimamisha matiti.

Kuna njia za asili ambazo zinaweza kutumika nyumbani. Mbinu hizi za nyumbani zina ufanisi mkubwa. Hebu na tuzichunguze baadhi ya mbinu za nyumbani za kusimamisha matiti ili uanze leo kurejesha urembo wako wa asili.

Mbinu za Nyumbani za Kusimamisha Matiti

1.Masaaji kwa kutumia Gel ya Aloe Vera au Mafuta ya Mlozi yaani almond

Aloe vera ina viambata ambavyo vinafanya kazi ya kukaza ngozi. Alo vera imekuwa ikitumika kwa karne nyingi ili kuondoa mikunjokunjo kwenye ngozi. Kufanya masaaji na aloe vera kutahakikisha kuwa gel ya aloe vera inapenya ndani ya ngozi na kuifanya ngozi kukaza. Masaaji pia huimarisha misuli ambayo inasimamisha matiti. Unaweza pia kutumia mafuta ya mlozi ama almons ambayo huongeza mzunguko wa damu. Mzunguko bora wa damu utafanya mishipa ya damu kuvimba na kusimamisha matiti.

2.Lishe kwa ajili ya kusimamisha matiti

Lishe ni muhimu sana katika kupata matiti yaliyosimama vizuri. Hii ni kwa sababu matiti yanashikiliwa na misuli ambayo inahitaji kukaza ili kusimamisha matiti. Misuli itakaza na kuwa imara ikiwa utatimiza mahitaji ya protini ya misuli. Pia inahitaji virutubisho muhimu kama vitamini, kalsiamu na madini. Unaweza kupata yote haya katika nyanya, kabichi, kimea, brokoli, karoti, nyama nk. Lakini pamoja na hii, unahitaji kupunguza unywaji wa kafeini inayopatikana kwenye kahawa na energy na kuacha kuvuta sigara.

3.Tango na Yai

Imeonekana kuwa tango inaweza kufanya ngozi kuwa imara. Hii ndio sababu hutumiwa kama mask ya uso katika matibabu ya urembo. Yai linajumuisha madini na virutubisho vingi. Vitu vyote hivi pamoja vinaweza kutoa virutubisho vingi kwa misuli iliyoko chini na kuimarisha ngozi.

Hii kwa kawaida itasimamisha matiti yako. Hivyo tumia mchanganyiko wa tango na yai kwenye matiti na karibu nayo kila siku. Acha mchanganyiko ukae angalau nusu saa baada ya hapo, safisha kwa maji ya baridi. Utakapojitazama ndani ya wiki moja, utaona mabadiliko.

4.Mafuta ya Mzeituni ama olive

Haya ni moja ya mafuta bora yanayopatikana kokote duniani, na yanafahamika zaidi kama mafuta matakatifu. Mafuta yana thamani kubwa sana kwenye mzunguko wa damu na afya ya moyo. Pia tafiti zimeonesha ya kuwa mafuta ya mzeituni yanaweza kuimarisha ngozi na kufanya iwe imara.
Kwa hiyo, masaaji matiti yako na mafuta ya mzeituni kila siku na utaona maboresho ndani ya siku chache.

5.Kuogelea

Kitendo cha kuogoelea nusu saa ndani ya bwawa mara kwa mara inaweza kufanya matiti yako yasimame kama hakuna kitu kingine. Kuogelea kunaimarisha misuli inayosaidia kushikilia matiti yako. Jiwekee ratiba ya kufanya mazoezi ya kuogelea mara kwa mara.