Njia 6 za Kupunguza Cholesterol bila dawa

Moja ya matatizo yanayojitokeza kwa kawaida kwa binadamu ni kongezeka kwa mafuta mabaya yaani bad cholesterol. Hata hivyo, cholesterol pia ni sehemu muhimu ya mwili wa binadamu katika uzalishaji wa homoni za mwili na shughuli zingine za mwili. Ndiomaana leo nataka nikwelekeze hatua simple za kupunguza cholesterol bila madawa wala mazoezi.

Kumbuka kuna aina mbili za Cholesterol, yaani cholesterol nzuri (HDL) na cholesterol mbaya(LDL). Pale cholesterol mbaya inapozidi kwenye mwili ndipo unaanza kupata magonjwa ya moyo na presha kupanda.

Tiba za Nyumbani kupunguza Cholesterol

1.Kitunguu Saumu kwa Cholesterol

saumu

Kitunguu saumu, ambacho jina lake kisayansi ni Allium sativum, kinajulikana kwa harufu yake ya kipekee na kwa matumizi yake mbalimbali hasa kwenye lishe. Mbali na matumizi yake kama kiungo katika vyakula mbalimbali, kemikali inayoitwa Allicin iliyopo ndani yake inajulikana kuua bakteria na fungus.

Na zaidi ya yote, kitunguu saumu kimejulikana kupunguza viwango vya cholesterol kwa wagonjwa wenye viwango vya juu vya LDL. Ni vyema kuongeza kitunguu saumu kwenye lishe yako kila siku, kutokana na faida nyingi za matibabu ambazo kitunguu saumu hutoa, pamoja na manufaa yake hakikisha unapunguza na ulaji wa vyakula vya sukari.

2.Tangawizi kupunguza Cholesterol

Tangawizi inaweza kutumiwa kama njia salama nyumbani kupunguza mafuta mabaya pamoja na matatizo mengine ya kiafya.Pia tangawizi kama tiba ya nyumbani kwa cholesterol, inaweza kutumiwa kwa njia mbalimbali, kama vile kutumiwa kama unga wa tangawizi na kuongezwa kwenye chai, ambayo sio chaguo tu la afya. Tangawizi inaweza pia kuongezwa kwenye supu, ambapo vipande vya tangawizi vinaweza kuchemshwa kwenye maji ili kutoa ladha nzuri kwenye supu yako.

3.Green tea kupunguza Cholesterol

green tea kupunguza cholesterol

Tiba ingine ya kuaminika na salama kwa cholesterol ni green tea. Green tea, inayojulikana kwa faida lukuki za kiafya, pia inafanya kazi vizuri kwa kesi ya cholesterol, kupitia mchakato wake wa kuongeza utoaji wa mafuta.

Zaidi ya hayo, green tea pia imegundulika kuzuia uzalishaji wa kiambata kinayodhaniwa kusababisha au kuchochea kusinyaa kwa mishipa ya damu, hivyo kuwa na matokeo ya moja kwa moja kwenye shinikizo la damu. Green tea pia ni kiondoa sumu chenye nguvu, ambacho kinadhibiti sumu hatari. Tumia green tea kila siku asubuhi kikombe kimoja, ili upate matokeo mazuri.

4.Tangawizi na uwatu kwa Cholesterol

Uwatu umekuwa ukitumika kwa muda mrefu na kupunguza kiwango cha cholesterol. Unaweza kupata tiba sahihi za nyumbani kwa cholesterol kwa kuweka nusu kijiko cha mbegu za uwatu kwenye kijiko cha majani ya ndimu na nusu kijiko cha tangawizi, kisha changanya vyote kwenye maji na uyachemshe. Baada ya mchanganyiko huu kuchemka, acha upoe kisha kunywa kikombe kimoja mara mbili kwa siku kwa kupunguza kiwango cha cholesterol.

5.Karanga kwa Cholesterol

Tiba rahisi na tamu ya nyumbani kwa cholesterol ni kula karanga kila siku. Karanga ni nzuri, zina virutubisho, tamu na zina ufanisi katika kupunguza viwango vya cholesterol kwenye damu. Unaweza kuchagua kati ya aina nyingi za karanga na zote ambazo zinakadiriwa kuwa na matokeo sawa kwenye viwango vya cholesterol kwenye damu.

Mbali na jukumu la kupunguza cholesterol, karanga pia zinahusika katika kupunguza triglycerides, na hatimaye, zina matokeo mazuri kwa watu wenye magonjwa ya moyo. Kiwango sahihi cha karanga cha kula kila siku kimekadiriwa kuwa takriban kiganja kimoja cha mkono.

6.Asali kwa Cholesterol

Tiba moja rahisi ya nyumbani kwa cholesterol ambayo haitakugharimu pesa nyingi ni kutumia asali. Unaweza kuweka kijiko kimoja cha asali katika kikombe cha maji ya moto ili kutengeneza kinywaji cha moto kinachoweza kufanya maajabu kwa viwango vya juu vya cholesterol. Asali ni dawa bora ya asili ambayo wat wengi hawaijui.