Baridi yabisi kitaalamu Arthritis ni hali ya maumivu ambayo inaweza kuzuia utendaji kazi wa mwili na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watu wanaosumbuliwa na hali hiyo.
Watu wanaosumbuliwa na baridi yabisi yaani arthritis huathiriwa kisaikolojia sana. Kupungua kwa uwezo wako kufanya kazi na kujinyoosha kama ilivokuwa hapo awali sio tu inaathiri maungo ya mwili bali pia akili kuvunjika moyo, kuchoshwa, na kukatishwa tamaa.
Hata hivyo, jambo la kwanza ambalo watu wenye arthritis wanahitaji kujua ni kwamba kuna tiba asili zinazopatikana nyumbani, endapo utazitumia kwa usahihi utapona. Kumbuka kwamba hakujapatikana tiba ya kudumu ya arthritis ambayo imegunduliwa na sayansi hadi sasa.
Tiba ya hospital
Tiba kubwaa ya hospital ni vidonge vya kumeza miaka yote na upasuaji wa kubadilisha viungo, ambao una kiwango kikubwa cha mafanikio. Walakini, upasuaji unaweza kuachwa kama njia ya mwisho, tunatumaini maendeleo zaidi katika sayansi yatawabariki watu ambao viungo vyao vinaweza kuwa vimeathiriwa.
Lakini, arthritis ni hali inayoweza kutibiwa kwa tiba mbadala. Kwanza, unatakiwa kujua kwamba haupo peke yako, ndiomaana tumeleta makala hii ikutoe kwenye mateso ya mda mrefu.
1.Punguza uzito mkubwa na kitambi
Ni muhimu kwa wagonjwa wa baridi yabisi kufanya jitihada za kupunguza uzito. Unapaswa kutafuta mpango bora wa kupunguza uzito ambao unaweza kufaa mahitaji na hali yako ya kiuchumi.
Kupunguza uzito kunapunguza mgandamizo kwenye viungo vyako, na kupunguza mgandamizo kwenye viungo kunapunguza msongo ambao viungo vyako vinaweza kuvumilia, haswa kama tatizo lipo zaidi kwenye magoti. Magoti ndiyo hupokea mgandamizo mkubwa kutokana na uzito wa mwili na kupunguza uzito ni tiba muhimu ya asili kwa arthritis.
Fuatilia lishe kupunguza uzito ukiwa na baridi yabisi
Wagonjwa wengi wa baridi yabisi hawawezi kufanya mazoezi kutokana na maumivu. Kwahivo hakikisha njia unayotumia kupunguza uzito isiwe ya mazoezi bali iwe ya kutumia lishe. Na kwenye lishe hakikisha unapata mtaalamu wa lishe mwenye uzoefu wa mda mrefu akwelekeze.
2.Kutibu baridi yabisi Kutumia Mchanganyiko wa Chumvi ya Moto.
Hii ni njia rahisi ya kutibu arthritis nyumbani. Unahitaji kuchukua kiasi cha kiganja cha chumvi ya mawe na kuipasha hadi ipate joto ambalo unaweza kuvumilia. Funika chumvi ya moto kwenye kipande safi cha kitambaa. Inapaswa kuwa moto sana ili uweze kuweka kwenye magoti yako, lakini sio kwa muda mrefu sana.
Chumvi kwa ujumla hutumiwa kama dawa ya kutuliza maumivu katika hali nyingi, na itakuwa na manufaa kwa kupunguza maumivu katika kesi ya baridi yabisi. Endelea kusugua kipande cha kitambaa kilicho na joto karibu na viungo vilivyovimbaa na ili upate nafuu ya papo hapo.
3.Kuoga Baharini kwa Ajili ya baridi yabisi.
Bahari ina uponyaji kutokana na uwepo wa chunvichumvi. Napendekeza kuoga katika maji ya bahari mara kwa mara walau mara 3 kwa week, kama unataka upate matokeo mazuri zaidi. Maji yenyewe yana nguvu ya kuponya, pia mchanga wake uliolowana una nguvu zaidi ya kuponya.Kwahivo kama huwezi kuogelea basi tembeea pembezoni mwa bahari ukanyage ule mchanga wenye majimaji., utapata nafuu ya papo hapo kutokana na maumivu yako.
4.Mafuta ya Mnyonyo kwa Ajili ya Arthritis
Mafuta ya nyonyo ama castor, ni tiba nzuri ya nyumbani kwa arthritis. Mbali na matumizi mengine mengi ya mafuta ya mnyonyo, pia yanaweza kutumika kwa masaaji kwenye maeneo yaliyoathiriwa na baridi yabisi. Mafuta ya mnyonyo yaliyopashwa moto vizuri yanapaswa kutumiwa kwa utaratibu kwenye viungo vilivyoathiriwa na kufanyiwa masaaji. Fanya zoezi hilo walau asbhi na jioni kwa week mbili uone mabadiliko makubwa sana.
5.Tumia Manjano kutibu baridi yabisi
Manjano ni dawa ya kushangaza ambayo inaweza kuwa na matokeo makubwa kwa afya yetu kwa ujumla, na ina viambata vingi ambavyo vinasaidia katika kutibu magonjwa mbalimbali. Manjano pia ina faida katika matibabu ya arthritis, ambapo unaweza kuchanganya unga wa manjano katika maji ya joto na kunywa mara kwa mara kwa kupunguza maumivu.
Manjano yamejulikana kwa muda mrefu katika mifumo ya dawa ya asili ya India na China kama njia kubwa ya kupambana na kuvimba ndani ya mwili, ambao unaweza kuleta manufaa katika matibabu na baridi yabisi. Unaweza pia kutengeneza mchanganyiko wa unga wa manjano na mafuta ya nazi na kuutumia kwenye maeneo yaliyoathiriwa, kwenye ngozi karibu na viungo vilivyoathiriwa.
Vyakula vya Kuepuka endapo unaugua baridi yabisi
Unatakiwa kuepuka matumizi ya vyakula hivi kama unataka kupona mapema
- Vyakula vya ngano kama mikate, chapati nk
- Vyakula vilivypikwa kwenye mafuta ya kuchemshwa mara kwa mara
- Vyakula vilivyosindikwa na kukobolewa sana
- Bidhaa za maziwa