Tiba mbadala ya kupasuka miguu

kupasuka miguu

Kupasuka miguu ni tatizo kubwa linalowatokea wanaume na wanawake pia. Shida inaanza si si tu kutokana na hali ya hewa kavu, bali pia ni ishara ya ugonjwa flani unaoendelea ndani ya mwili . Wanawake wako katika hatari kubwa ya kuwa ya kupasuka miguu kwani miguu yao mara nyingi inaambukizwa na vumbi na hali mbaya ya hewa. Ni nadra sana mtu kujali miguu kama wanavyojali ngozi ya uso wakati wa huduma za urembo.

Migu iliyopasuka inaweza kuwa na maumivu na vinaweza kuonekana kama kitu kibaya. Pia miguu ikipasuka inaweza kuharibu uzuri wa muonekano wako mzima ikiwa hautachukua hatua mapema kutibu. Leo nimekandikia tiba rahisi ambazo waweza kuzitumia ukiwa nyumbani kwako kutibu tatizo kabla ya kwenda hospitali.

Hizi hapa tiba mbadala za kupasuka miguu

1.Usafi wa miguu

Huduma ya miguu inaanza na kunawa na kusugua miguu yako kwa maji ya uvuvvgu ili kuondoa uchafu wote mara tu unapokuwa nje. Maji ya moto husaidia kulainisha miguu. Lazima usafishe miguu yako vizuri kabla ya kwenda kulala.

2.Mafuta ya Mzeituni

olive oil

Chukua siki ya apple cider na mafuta ya mzeituni kwa uwiano sawa. Changanya vizuri na uhifadhi kwenye chupa ya glasi. Paka kwenye miguu yako kila siku usiku na vaa soksi ili suluhisho liweze kufanya kazi vizuri. Tiba hii hupunguza rangi na husaidia kuzifanya nyufa kwenye visigino kuwa laini. Hakikisha miguu yako iko safi kabla ya kutumia tiba hii.

3.Gliserini

Gliserini ni mafuta ya asili ya unyevu na inasaidia kuharakisha mchakato wa uponyaji wa visigino vilivyovunjika. Tengeneza suluhisho lenye sehemu moja ya gliserini, sehemu moja ya juisi ya limau, na sehemu mbili za maji ya waridi. Hifadhi kwenye chupa na tumia kadri unavyohitaji. Hii ni tiba nzuri kwa visigino vilivyopasuka na unaweza kuitumia kipindi chote cha majira ya baridi ili kuweka miguu yako vizuri.

4.Asali kutibu kupasuka miguu

asali

Asali inaweza kufanya kazi vizuri kama tiba mbadala wa mipasuko kwenye miguu. Tafiti zinasema kwamba asali inaweza kusaidia kutibu na kuponyesha kidonda mapema, pia asali inafanya ngozi kwa nyororo. Tumia asali kama scrub kwenye miguu yako kila siku kwa nus saa. Pia unaweza kupaka usiku kabla ya kulala na kuvaa sox mpaka asbuhi.

5.Mafuta ya nazi

mafuta ya nazi

Mafuta ya nazi yanashariwa kutumika kwa matatizo yote ya ngozi ikiwemo aleji ya ngozi, magamba kwenye ngozi na hata kupasuka kwa miguu yako. Tumia mafuta haya kila siku asubuhi na jioni baada ya kuoga kwa mwezi mmoja na uone maajabu yake