Tiba mbadala ya mafua na Kikohozi cha Mtoto

Mafua na kikohozi cha mtoto unavuruga na kuleta mabadiliko katika mfumo wake wa kulala hasa pale mafua yanapotoka mara kwa mara, kumbatana na homa. Hii inaweza kukufanya wewe pia kama mzazi kuwa na wasiwasi.

Wamama wengi huanza kuhangaika wanapoona watoto wao wanapata homa na hata kwa kikohozi cha kawaida. Wanahangaika kwenda famasi kununua dawa. Lakini nipo hapa kukupa tumaini, kwamba huhitaji kukimbia duka la dawa haraka,, kwani kuna njia kadhaa za kawaida na salama za nyumbani ambazo zinaweza kutumika kutibu kikohozi na mafua kwa watoto. Njia hizi ni salama na hupunguza usumbufu na gharama za kwenda hospitali mara kwa mara.

Mbadala ya Nyumbani kwa Mafua na Kikohozi cha Mtoto

1.Asali

Asali ni dawa ya kufubaza kikohozi na mafua na tiba rahisi ambayo inaweza kutibu kikohozi na kuvimba koo. Chukua chupa ya kulisha mtoto na jaza nusu yake na maji ya uvuguvugu. Weka nusu kijiko cha asali, tingisha mpaka ichanganyike na maji kisha mpe mtoto anywe. Asali haipendekezwi kwa watoto walio chini ya mwaka mmoja kwani inaweza kuwa na chembechembe za botulinum ambazo zinaweza kuwa hatari. Kumpa mtoto asali mara mbili kwa siku kunaweza kusaidia kupunguza mafua makali na kukata kikohozi bila hata kwenda duka la dawa.

2.Matone ya chunvi

Matone ya chunvi yatasaidia kusafisha njia za pua za mtoto na kuondoa makamasi yaliyokwama na kuganda ambayo yanaweza kusababisha mtoto kupata shida katika kupumua. Chukua kijiko 1/4 cha chumvi na uweke kwenye kikombe kimoja cha maji, kisha koroga kupata mchanganyiko mzuri. Chukua vidole vyako kisha dondosha matone kiasi kwenye pua zake. Rudia hadi mtoto apige chanya njia za pua ziwe wazi vya kutosha kwa mtoto kupumua.

3.Tangawizi

tangawizi

Tangawizi ni tiba yenye ufanisi katika kutibu kikohozi, mafua makali. Inasaidia kuongeza mzunguko wa damu na pia kuufanya mwili upate joto ili makamasi yaweze kuyeyushwa na kutolewa. Kwa watoto wachanga, tengeneza chai kwa kuongeza gramu tano za tangawizi kwenye kikombe kimoja cha maji yanayochemka.

Subiri kwa dakika kumi na kisha ongeza nusu kijiko cha asali. Baada ya kufikia joto la kawaida, jaza nusu chupa na mpe mtoto aweze kunywa. Tangawizi ni muhimu sana katika kutibu kikohozi kwa watoto, hivo usikose kiungo hiki muhimu ndani kwako.

4.Kitunguu saumu kutibu mafua na kikohozi cha mtoto

Kitunguu saumu ni kiungo kilichopo kwenye kundi la antibacterial ambalo husaidia kuangamiza bakteria wa kikohozi. Unaweza kutayarisha chai ya kitunguu saumu kwa kuweka vipande vilivyokatwa vya vitunguu saumu 2 kwenye kikombe kimoja cha maji yanayochemka. Acha kwa dakika kumi na ruhusu kufikia joto la kawaida. Unaweza kumpa mtoto chai hii kwa kiasi kidogo kila siku. Ongeza kijiko cha asali ikiwa mtoto wako ana umri zaidi ya mwaka mmoja .

5.Manjano

manjano kutibu mafua na kikohozi cha mtoto

Weka kiwango kidogo cha manjano walau kijiko kimoja kwenye juisi ya kawaida ya matunda au maziwa au hata maji ya uvuguvugu anayokunywa mtoto wako. Na hii inaweza kutolewa mara mbili kwa siku ili kuondoa kikohozi na mafua. Manjano husaidia kuondoa uvimbe, bakteria na pia kuimarisha mfumo wa kinga ya mtoto kupambana na maambukizi.

6.Limau

Limau ni dawa ya antibacterial na antiseptic inayoweza kutumika kutibu kikohozi na mafua. Limau pia lina kiwango kikubwa cha vitamini C ambacho husaidia katika kuimarisha kinga ya mwili. Chukua maji ya vuguvugu kikombe cha chai, kamulia limau moja kubwau na ongeza kijiko cha asali kwa ajili ya watoto wakubwa. Mpe mtoto kwa kiasi kidogo kwa kuongeza maji ya kutosha. Hii ni tiba rahisi, salama yenye ufanisi sana ambayo inaweza kutolewa kwa watoto walio na kikohozi na mafua makali.