Tiba mbadala ya Mba na ukurutu wa Kichwa

mba na ukurutu

Mba na ukurutu wa kichwa ni moja ya matatizo yanayokabili ngozi kwa watu wengi sana. Tatizo linajionesha hasa wakati wa kuchana nywele zako, pale vitu vyeupe vinapotoka kichwani mwako. Mba na ukurutu wa kichwa inaweza kukufanya usijiamini mbele za watu na kukosa raha.

Ingawa mba na ukurutu wa kichwa unaweza kuonekana katika misimu yote, imegunduliwa kuwa ukali wa mba na ukurutu wa kichwa huwa unatofautiana kulingana na msimu na mara nyingi ni mbaya zaidi wakati wa baridi kuliko ilivyo katika majira ya joto.Nimekwandalia tiba mabadala za nyumbani kwako ambazo ni hakika zinatibu tatizo lako endapo utafatilia kwa umakini.

Tiba mbadala za Nyumbani kwa Mba na ukurutu wa Kichwa

1.Limau

Limau inaaminika kuwa na ufanisi katika matibabu ya mba na ukurutu wa kichwa. Njia bora ya kutumia limau ni kukamulia ndimu kwenye mafuta ya nazi,pasha kidogo huo mchanganyiko na upake kwa taratibu kwenye kichwa. Kupaka mafuta ya nazi na ndimu kwenye kichwa mara kwa mara husaidia katika kusafisha ngozi na kutoa seli za ngozi zilizokufa. Kupaka na kusugua kwa mafuta ya nazi kwenye kichwa, mbali na kuongeza mzunguko wa damu, pia husaidia kuondoa vipande vya ngozi na kusafisha eneo hilo, hivyo kupunguza uundaji wa mba na ukurutu wa kichwa.

2.Aloe Vera

Aloe Vera ni dawa ya maajabu na asili ambayo inaweza kusaidia kushughulikia matatizo na magonjwa mengi ya kiafya. Jambo zuri kuhusu Aloe Vera inafanya kazi kwa ndani na kwa nje pia. Poda ya Aloe Vera ambayo inapatikana zaidi kama gel, inaweza kutumiwa kwenye ngozi na kusugua kichwa ili kutib mba na ukurutu wa kichwa.

Matumizi: Chukua poda yaaloe vera, ama hata majimaji yake, pakaa kwenye kichwa, funika kichwa chako na auche kwa nusu saa. Osha kwa maji ya vuguvugu kisha jipake mafuta ya nazi. Pia unaweza kunywa juisi ya Aloe Vera ambayo imepnguzwa makali, itakusaidia sana kuimarisha afya ya ngozi.

3.Masaaji kwa Mafuta

Kichwa kinahitaji kusuguliwa pamoja na mafuta kwa kawaida, na kuna aina nyingi za mafuta asili yanaweza kutumika kusugua kwenye kichwa. Baadhi ya mafuta yanayofaa ni pamoja na mafuta ya nazi, mafuta ya sesame na mafuta ya mzeituni. Mafuta haya yanaweza kuyeyushwa kidogo na kupakwa kwenye kichwa kisha kusuga kwa nusu saa. Kisha unaweza kunawa kichwa chako kwa maji ya uvuguvugu yaliyochanganywa na vinegar ya apple. Matumizi ya kawaida ya mafuta haya huchukuliwa kama tiba ya nyumbani inayofaa kwa mba na ukurutu wa kichwa.

4.Mafuta ya Mzeituni kutibu mba na ukurutu

Ni muhimu kudumisha kiwango sahihi cha unyevu kwenye kichwa ili kuzuia mba na ukurutu wa kichwa. Mafuta ya mzeituni yanajulikana kwa matokeo yake ya kuimarisha unyevu kichwani. Chukua mafuta kidogo ya mzeituni na kuyapaka kwenye kichwa kabla ya kulala usiku. Unaweza kusafisha mafuta hayo kwa kutumia maji ya uvuguvugu yaliyochangwa na apple vinegar asubuhi kama tiba nzuri ya nyumbani ya mba na ukurutu wa kichwa.

5.Mafuta ya almond

Almond imejulikana kwa muda mrefu kwa wezo wake kama dawa ya magonjwa mbalimbali , na mafuta ya almond pia yanachukuliwa kuwa mazuri kwa mizizi ya nywele. Paka mafuta ya almond yaliyochanganywa na mafuta ya nazi, acha kwa muda na suuza.

Lishe na Mtindo wa Maisha kwa Mba na ukurutu wa Kichwa

Lishe

Ingawa hatua hizi za hapo juu zitasaidia sana katika kudhibiti mba na ukurutu wa kichwa kwa njia ya asili, ni muhim pia kulo lishe kamili ili kuweka wiano mzuri wa virutubishio mwilini mwako. Punguza ulaji wa vyakula vilivyokaangwa, vyakula vya sukari, pamoja na vyakula vilivyosindikwa, na badala yake jikite katika chakula cha asili mboga mboga na matunda.

Kula matunda safi na mboga za kijani, mbegu zilizoota, kutafuna karanga mbichi, na kutumia nafaka ambazo hazijakobolewa ni baadhi ya mbadala wa asili ya mba na ukurutu wa kichwa.