Maambukizi ya kibofu, maarufu kama UTI husababishwa hasa na bakteria. Dalili za maambukizi ya kibofu ni kuhisi kuwaka moto wakati wa kukojoa, mkojo wa mawingu au njano sana na maumivu ya tumbo. Endapo maambukizi yameenea sana, mtu anaweza kupata joto kali la mwili, kutetemeka, kichefuchefu, maumivu ya mgongo, na kuhara.
Kwenye tiba za kisasa endapo umeugua UTI, unatumia antibiotics za duka la madawa. Lakini pia habari njema ni kwamba kuna mbinu za nyumbani ambazo mara nyingi wengi wanadharau lakini ni salama na zenye ufanisi zaidi. Nitakufndisha tiba za UTI bila kwenda hospital kiwa nymbani kwako.
Je UTI inaweza kuathiri mirija ya mkojo?
Jibu ni ndio, maambukizi ya bakteria kwenye kibofu yanaweza pia kusambaa kwenye mirija inayopitisha mkojo kitaalam tunaita urethritis, ambayo ni ugonjwa wa kuta za mkojo. Katika kesi kama hizo, mgonjwa anateseka kutokana na kukojoa kwa kuwaka moto, kwani bomba ambalo mkojo unapita linakuwa limevimba.
Je figo laweza kuathiriwa na UTI?
Figo pia hazipo salama endapo umeugua uTI sugu, bakteria wanapoathiri figo, unapata tatizo kitaalam tunaita pyelonephritis. Katika aina hii ya maambukizi, bakteria huvuka kibofu na kuanza kuathiri figo. Hutokea hasa wakati mgonjwa ameugua kwa mda mrefu bila kutibiwa.
Chanzo cha Maambukizi ya UTI
Kabla hatujajadili mbinu za ufanisi ambazo zitasaidia kupona UTI ukiwa nyumbani, tuelewe sababu za maambukizi ya uti.
Wanawake wanaweza kupata maambukizi baada ya kushiriki tendo la ndoa. Katika kesi kama hizo, bakteria wanaweza kufika kwenye kibofu kupitia kuta za mkojo na kusababisha maambukizi ya kibofu. Pia kondomu inaweza kusababisha maambukizi kwa wanawake. Kwa wanaume, maambukizi yanaweza pia kusababishwa na tendo la ndoa lisilo salama na kutoknywa maji ya kutosha.
Tiba mbadala za Nyumbani Kutibu UTI
Wakati mtu anachagua mbinu za nyumbani za kutibu maambukizi ya kibofu, lazima awe na subira na kuruhusu tiba ya asili ifanye kazi kwa ufanisi.
1.Juisi ya Tango
Juisi ya Tango Inajulikana kwa kuwa na matokeo chanya kwenye kutibu UTI, mtu anaweza kunywa juisi ya tango angalau mara tatu kwa siku kutibu maambukizi ya kibofu. Changanya kijiko cha asali na juisi ya limau kwenye juisi ya tango na utapata tiba ya asili ya maambukizi ya kibofu.
2.Majani ya Mchicha
Mchicha uliosagwa vizuri na maji ya nazi safi unaweza kutibu maambukizi ya kibofu kwa ufanisi. Ufanisi unatokana na madini ya nitrate na potasiamu ya mchicha ambayo husafisha mkojo.
3.Limau kutibu UTI sugu
Changanya juisi ya limau na maji ya uvuguvugu, kisha achia mchanganyiko huo upoe na kunywa kidogo kila baada ya masaa mawili. Hii inajulikana kupunguza maumivu unayohisi unapopatwa na maambukizi ya kibofu.