Njia za Asili za Kutibu Uchafu ukeni
Uchafu ukeni kwa kiasi kikubwa ni jambo la kawaida kwa mwanamke. Uteute unaotoka unaotolewa na tezi za kwenye uke na shingo ya kizazi ili hukusanya seli zilizokufa, bakteria, na uchafu mwingine. Utokaji huu wa uchafu husaidia kusafisha uke na kuulinda kutokana na maambukizi.
Lakini wakati utoaji huu unakuwa mwingi sana, rangi nyeupe iliyochanganyika na manjano na una harufu mbaya, basi ujue kwamba siyo uchafu wa kawaida. Uchafu huu unaweza kuwa unasababishwa na maambukizi ya bakteria, fangas au hata virusi. Mabadiliko katika uwiano wa bakteria katika uke husababisha maambukizo na kusababisha mabadiliko katika muundo, rangi na harufu ya utoaji.
Magonjwa ni chanzo kikubwa cha Uchafu ukeni
Uwiano wa bakteria ukeni unaweza kuvurugika kutokana na sababu kadhaa kama magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana, kansa ya shingo ya kizazi, kisukari, ngono zisizo salama na zisizo na mpangilio na dawa fulani kama vidonge vya uzazi, na antibiotics. Sehemu ya nje ya uke inakuwa imevimba na kusababisha kuwashwa sana ndani na karibu na uke. Dalili zingine mbaya waweza kupata ni maumivu na kuwaka wakati wa kukojoa na tendo la kujamiiana pia linakuwa la maumivu.
Njia Madhubuti za Kutibu Uchafu ukeni kwa tiba za asili
1.Maji ya Mwarobaini
Chemsha sufuria ya maji na weka kundi la majani ya mwarobaini yaliyotwangwa vizuri. Chemsha kwa dakika tano kisha zima moto. Maji yakipoa, chuja na osha uke wako kupitia haya maji mara tatu au nne kila siku. Mwarobaini utaondoa bakteria hatari haraka bila kuharibu bakteria wazuri na utarejesha uwiano wa bakteria kwenye uke. Pia utapunguza uvimbe na kuwasha na kuleta nafuu kwa maumivu.
2.Siki ya apple(apple cider vinegar)
Siki ya apple ni tiba nyingine ya asili ambayo husaidia kuangamiza bakteria na fangasi hatari bila kuharibu bakteria wazuri mwilini. Chukua kijiko kimoja cha siki ya apple na kichanganye na maji ya uvuguvugu. Osha uke wako na suluhisho hili mara tatu au nne kila siku. Siki ya apple itarejesha uwiano wa pH kwenye ngozi ya uke na karibu na uke na kuondoa maambukizo kwa haraka. Pia itapunguza kuwasha na kuwaka moto.
3.Majani ya Dhania au corriander
Majani ya dhania yana harufu nzuri na yana uwezo mkubwa kitiba. Yana madini na vitamini muhimu na viambata vyenye nguvu za kuzuia bakteria, kuzuia fangasi, kupunguza uvimbe na kuondoa sumu. Loweka kundi dogo la majani ya dhania kwenye glasi ya maji usiku kucha. Asubuhi, chuja maji na unywe kwa tumbo tupu. Pia ongeza majani ya dhania yaliyokatwakatwa kwenye vyakula vyako vyote vilivyopikwa.
4.Majani ya Mpera
Majani ya mpera yana uwezo mkubwa sana kwenye tiba asili. Yana sifa za kuzuia bakteria, kupunguza uvimbe na kuwa na kuondoa sumu mwilini. Jinsi ya kutumia ili kutibu uchafu ukni: Chemsha majani manne ya mpera yaliyosagwa kwenye glasi ya maji kwa dakika tatu au nne. Chuja maji kisha kunywa nunu kikombe mara tatu kila siku kwa wiki moja.